Saturday, November 28, 2020

NI JUKUMU LA KLABU SASA KULINDA VIPAJI U-20

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SELEMANI ALLY, TSJ

MICHUANO ya vijana iliyoshirikisha timu za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya umri wa miaka 20 (U-20), imemalizika kwa Simba kuchukua ubingwa msimu huu.

Vijana hao wa Simba walichukua ubingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 5-3, baada ya kutoka sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 dhidi ya wenzao wa Azam katika mchezo wa fainali uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Fainali hiyo ilikuwa ya ushindani mkali kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kuonyesha kiwango cha hali ya juu huku zikicheza soka ya kufundishwa.

Michuano hiyo iliandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa lengo la kuwapa uzoefu wa kucheza  wachezaji wa vikosi vya vijana kwa klabu za Ligi Kuu Bara.

Naamini kwamba, vipaji vingi vimeonekana kupitia michuano hiyo, iliyoanza hatua ya makundi na baadaye fainali.

Ni jukumu la makocha wa timu hizo za  vijana zilizoshiriki michuano hiyo kuendelea kuvilea vipaji chipukizi vya wachezaji walioonyesha viwango ili baadaye waweze kuwa tegemeo katika vikosi vyao.

Viongozi wa klabu wanatakiwa kuendelea kuwapa mahitaji wachezaji ili makocha waweze kuendelea kuwafundisha, kwani bila timu za vijana soka la Tanzania haliwezi kupiga hatua.

Ni ukweli usiopingika kwamba, timu za klabu na Taifa zinaundwa kwa kuwepo msingi wa michuano ya vijana ambao wanakuwa wameandaliwa vizuri.

Timu za vijana ni uti wa mgongo wa soka katika taifa lolote ambalo limepiga hatua kisoka, hivyo vijana hao wasiishie mitaani kwani wanatakiwa kuendelea kujengwa.

Pamoja na baadhi ya timu kuishia njiani katika michuano hiyo, lakini waliweza kuonyesha vipaji vyao na wakiendelea kulelewa, hakika baada ya miaka mitano ijayo soka ya Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa.

Natarajia kuona wachezaji walioshiriki michuano hiyo baada ya miaka mitano watakuwa wametoka hapa walipo na kwenda kucheza soka ya kulipwa katika klabu mbalimbali barani Afrika na Ulaya ili baadaye waje kuunda kikosi bora cha Taifa ‘Taifa Stars’.

Kielelezo tosha ni Thomas Ulimwengu ambaye alitokea katika timu ya vijana chini ya miaka 17 maarufu Copa Cocacola kabla ya kulelewa katika Kituo cha Tanzania Soccer Academy (TSA), kilichokuwa kikimilikiwa na TFF na kusajiliwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ulimwengu kwa sasa ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Taifa Stars, licha ya msimu huu kutemwa katika kikosi za mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.

Lakini wachezaji kama Simon Msuva wa Yanga, aliibuliwa katika michuano ya vijana na sasa ni tegemeo kwenye kikosi hicho.

Wachezaji hao ni mfano tosha kwa vijana wenzao ambao wameonekana kuchipukia kwenye michuano hiyo iliyomalizika wiki iliyopita.

Itakuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu kama wachezaji hao chipukizi walionekana katika michuano hiyo hawataendelea kujengewa misingi bora ya kukuza vipaji vyao.

Pamoja na changamoto nyingi zinazozikabili klabu kwa kutokuwa na miundombinu bora ya viwanja, uwezo wa kuendesha timu zao, kuna kila sababu ya kuchukua uamuzi wa makusudi ya kuwa na timu endelevu za vijana zenye umri tofauti.

Naamini kwamba, klabu zikifikia kukabiliana na changamoto hizo, hakika kiwango cha soka kinaweza kubadilika kwa muda mfupi.

Lakini shirikisho la soka nchini, linatakiwa kuwa na programu endelevu kwa timu za vijana kwa kuwa na michuano mingi inayozingatia umri ili kuweza kutengeneza soka.

Michuano ya vijana isiishie msimu mmoja, kwani viongozi wenye dhamana na soka la Tanzania, wanatakiwa kuhakikisha klabu inakuwa na timu endelevu ambayo ipoi tayari kushiriki michuano ya aina yoyote ambayo itakuwa imeandaliwa.

Ni matumaini yangu kwamba, michuano mingine ya vijana itaboreshwa zaidi, baada ya msimu huu kuwepo kwa dosari kubwa ikiwamo udanganyifu wa umri wa wachezaji, kwani baadhi ya klabu zilichezesha vijana waliovuka umri huo.

Sitarajii kuona upungufu uliojitokeza katika michuano ijayo, kama tunahitaji kujenga soka letu na kuwemo katika orodha ya klabu au timu za taifa zinazofanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -