Saturday, November 28, 2020

NI KLABU IPI ATAKAPOTUA SANCHEZ?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MSIMU huu straika Alexis Sanchez amekuwa katika kiwango kizuri cha uchezaji akiwa na klabu yake, ikilinganishwa na tangu mwaka 2014 alipojiunga na timu hiyo akitokea  Barcelona.

Lakini pamoja na kuwa katika ubora huo, maisha ya raia huyo wa Chile kwenye klabu hiyo ya Kaskazini yanaonekana kuwa ukingoni, ikiwa ni bado miezi 15 kabla ya mkataba wake kumalizika kutokana na kwamba bado hajamwaga wino katika mkataba mpya.

Hali hiyo inatokana na Sanchez kupagawa kutokana na Arsenal kushindwa kupiga hatua katika kipindi cha mwaka mmoja na huku akishinikiza kulipwa pauni 250,000 kwa wiki, kiasi ambacho kinaonekana kinaweza kuwa mtihani mkubwa kwa washika bunduki hao wa Kaskazini mwa jiji la London.

Kutokana na mvutano huo na licha ya kwamba  Sanchez wakati akiwa katika majukumu ya timu ya Taifa Chile kueleza wazi kwamba nia yake ni kuendelea kubaki jijini London, kuna klabu kubwa kadhaa ambazo zimemuweka njia panda ambapo patamfaa kwenda.

Katika Makala haya BINGWA imejaribu kuangalia timu zinazomwania nyota huyo na kama zitamfaa kupata kile anachokitaka au aendelee kukipiga Arsenal.

 Arsenal

Ikiwa inaonekana dhahiri  kwamba  Arsene Wenger  huenda akaendelea kuinoa  Gunners bada ya kuwapo na taarifa zinazoeleza kuwa Mfaransa huyo atapewa mkataba wa miaka miwili, licha ya kukaliwa kooni na mashabiki kabla ya ukweli kufahamika itakapofika mwishoni mwa msimu huu, kibarua cha kwanza kwa kocha huyo kitakuwa ni kumshawishi Sanchez abaki, iwe kwa kusaini mkataba mpya ama la.

Kwa sasa raia huyo wa Chile yupo kwenye mkataba unaomfunga hadi mwakani na hivyo Wenger hawezi kumruhusu kuondoka, hata kama hataki na mwisho wake watalazimika kukaa chini na kusikiliza kile ambacho Mfaransa huyo anakihitaji na si staa huyo kulazimisha kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Chelsea

Katika klabu hii, Arsene Wenger anaweza kujikuta ana kibarua kikubwa kutokana na kwamba staa huyo ameshatangaza kuwa kuna klabu moja tu jijini London anayoweza kuchezea, jambo ambalo linaonekana kuwa kuna uwezekano kwa Sanchez kutimkia Stamford Bridge.

Jambo hilo linaonekana kuwa wazi kutokana na kuwa endapo raia huyo wa Chile atataka kubaki jijini London na kutwaa mataji, anaweza kufanya hivyo endapo atakuwa chini ya Antonio Conte.

Jambo jingine ambalo linaweza kumfanya nyota huyo kutua kwenye klabu hiyo ni kutokana na kuwa Mwitaliano huyo ni shabiki wa  Sanchez kwa muda mrefu, kutokana na kuwa mwaka 201 alijaribu kumpeleka  Juventus  kutoka Udinese kabla ya kuzidiwa kete na Barcelona.

Hivyo kocha huyo anamtamani nyota huyo, lakini si kama kipindi ambacho  Arsenal walikuwa wakiwaachia wachezaji kwenda Manchester City, ama ilipomruhusu  Robin van Persie kwenda  Manchester United kutokana na kwamba kwa sasa hawana ukata wa kulazimisha kuuza wachezaji.

Juventus

Katika klabu hii hakuna tatizo la maisha nchini Italia, kutokana na kwamba Sanchez kwa muda mrefu amekuwa akifukuziwa na klabu hii ya mjini Turin, hususan kipindi ilipokuwa chini ya Conte.

Hadi sasa mabingwa hao wa michuano ya Ligi ya Serie A wana ndoto za kumpeleka nchini Italia na mara zote imekuwa ikimuona Sanchez kama mchezaji ambaye anaweza kuipaisha klabu hiyo ya Bianconeri.

Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kwamba licha ya Juve kulitawala soka la Italia na kuleta ushindani katika michuano ya Ulaya baada ya mwaka 2015 kufika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa, wanaweza kuongeza kasi katika mbio za kumwania nyota huyo.

Msimu uliopita vigogo hao walitumia kiasi kikubwa cha fedha kuwanasa mastaa kadhaa, wakiwamo Miralem Pjanic  na  Gonzalo Higuain, hivyo hawataweza kusita kujikamua kiasi kingine kuingia katika vita hiyo ya kumwania staa huyo.

Atletico Madrid

Klabu ya Atletico Madrid nayo inaripotiwa kufuatilia kwa karibu kuhusu hatima ya Sanchez katika klabu hiyo ya  Emirates na huku ikiwa na matumaini ya kumfanya staa huyo atue katika jiji hilo la Madrid.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya kwa sasa Atletico ipo katika kibano cha kutosajili ilichopewa kwa kuvunja kanuni za usajili baada ya kutiwa hatiani kwa kusajili wachezaji makinda.

Pamoja na hali hiyo, lakini kutokana na kuwapo na uwezekano wa kuondokewa na nyota wao, Antoine Griezmann, kikosi hicho kinaweza kupata kiasia kikubwa cha fedha kwa ajili ya kugharamia usajili huo wa Sanchez.

 Paris Saint-Germain

Vipi kuhusu kwenda Paris?

Msimu huu mabingwa hao wa Ufaransa walikuwa wanataka kufanya vizuri zaidi katika michuano ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, ndoto zao ziliyeyushwa na  Barcelona  na kwa sasa kocha wao, Unai Emery kukaliwa kooni na huku mipango yao ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 ikiwa haiendi sawa.

Kwa sasa Les Parisians bado wanasaka mbadala wa kuziba pengo la nyota wao wa zamani, Zlatan Ibrahimovic na wanamuona Sanchez ndiye anayeweza kuwafaa na wana uwezo wa kuweza kumudu bei atakayouzwa na mshahara anaoutaka na kumhakikishia maisha mazuri pindi atakapotua katika klabu hiyo ya jijini Paris.

Bayern Munich

Mabingwa hao wa Ujerumani ndio walioitupa nje Arsenal katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, bada ya kuwabugiza jumla ya mabao 10-2 na kumuacha Sanchez akiwa ameduwaa kutokana na kipigo hicho kutoka kwa wazee hao wa kazi wa the Allianz Arena.

Kwa sasa kuna tetesi kuwa Bayern wanaweza kurusha ndoana kwa Sanchez wakati wa usajili wa majira haya ya joto na pia ni kwamba licha ya Carlo Ancelotti kuwa na wachezaji kama Arjen Robben na Franck Ribery, hatima ya staa mwingine, Douglas Costa bado haieleweki na huku mipango ya kocha huyo kumpa mkataba wa kudumu Kingsley Coman ukionekana kuvurugwa na staa huyo kuwa majeruhi.

Kwa hiyo basi kwa kumuongeza  Sanchez  katika safu ya ushambuliaji akiwa na nyota wengine kama vile  Robert Lewandowski  na  Thomas Muller, inaweza kuwafanya tishio katika vita ya kuwania ubingwa wa Ulaya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -