Friday, November 27, 2020

NI KWELI WANAWAKE WAKIPENDA WAMEPENDA KWELI? -2

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KARIBUNI wasomaji wangu katika safu hii ya mahusiano ambayo huwajia kila Jumamosi na Jumanne ikilenga kufahamishana hili au lile kuhusiana na mambo ya mapenzi au ukipenda unaweza kuita mahaba.

Awali ya yote, niwashukuru wale wote ambao wamekuwa wakitumia muda na fedha zao kutuma ujumbe wenye lengo la kupongeza mada zinazotolewa katika safu hii, huku wengine wakichangia pale walipoona inafaa kufanya hivyo. Nasema ahsanteni sana.

Baada ya salamu hizo, tugeukie mada ya leo ambayo ni mwendelezo wa ile ya Jumanne ya wiki hii iliyouliza; ‘Ni kweli wanawake wakipenda wamependa kweli?’

Mada hiyo ililenga kufahamu ukweli juu ya mabishano yanayoendelea huko mitaani kwamba kati ya wanawake na wanaume ni akina nani wenye upendo wa dhati kwa wenzao wao.

Baada ya mada ile, nilikaribisha maoni ya wasomaji ambapo wengi wameonekana kuigwaya kwa kushindwa kujibu swali na matokeo yake kusimulia visa vilivyowahi kuwatokea katika mahusiano na waliowaamini wanawapenda.

Hebu tupate baadhi ya maoni ya wasomaji juu ya mada hii kama nilivyoahidi Jumanne iliyopita.

“Mimi nawapa asilimia zote wanaume katika suala la mapenzi. Hakuna kiumbe mwenye roho nzuri kama mwanaume. Unampenda mwanamke kwa moyo wote lakini atakuja kukuudhi na kusahau yote mema uliyomfanyia. Nasema hivi kuna mwanamke nilimsaidia kwa hali na mali karibu mwaka mzima baada ya kutelekezwa na mpenzi wake alipojifungua. Yule bwana alishindwa kumhudumia kwani alikuwa na mke wake wa ndoa. Kutokana na ukata pale nyumbani yule mwanamke alitaka kuuza vyombo vyake vya ndani ili arudi kwao lakini kwa imani nikajitolea kumsaidia mpaka mtoto alipokaribia miaka miwili na nusu, lakini alichonifanyia baadaye alinitoroka,” anasema Mohammed Mohammed.

“Kiukweli wanaume hawana mapenzi ya kweli hata kidogo, wengi wao hutaka kuonja na kupita,” anasema Dora wa Musoma.

“Wapo wanaume hawana upendo wa kweli, unampenda kwa moyo wote kumbe yeye ni tapeli, ukijua hilo mahusiano yanavunjika tu ili usipoteze muda kwa mtu mwongo,” anasema Celine wa Arusha.

“Suala la kupenda ni bahati tu, ukimpata akupendaye kwa dhati kinyume chake, hakuna sisi wote waongo,” anasema Doa ambaye hata hivyo hakutaja sehemu alipo.

“Mimi nawapa asilimia zote wanaume katika suala la mapenzi. Hakuna kiumbe mwenye roho nzuri kama mwanaume. Unampenda mwanamke kwa moyo wote lakini atakuja kukuudhi na kusahau yote mema uliyomfanyia. Nasema hivi, kuna mwanamke nilimsaidia kwa hali na mali karibu mwaka mzima baada ya kutelekezwa na mpenzi wake alipojifungua,” anasema msomaji ambaye hata hivyo hakutaja jina lake.

Ndugu msomaji, imekuwa ikisisitizwa kuwa wanawake ndio vigeugeu katika suala zima la mapenzi kwani wengi wao si waaminifu hasa pale wanapokutana na vishawishi vya fedha, magari na nyumba za kifahari, kazi nzuri na mengineyo kama hayo.

Hao wanadai kuwa hata mwanamke umwonyeshe upendo kiasi gani, akikutana na mwanaume mwenye fedha chafu atakayemhakikishia kuishi katika nyumba ya kifahari, kutembelea gari la kifahari na mengine kama hayo, lazima atamsaliti mume au mpenzi wake.

Lakini kwa wanaume, imedaiwa kuwa wao hawatabiriki, wanaweza kuonyeshwa kila aina ya upendo na wake au wapenzi wao, lakini bado wakaendelea kujihusisha kimapenzi na wasichana wengineo, hasa wale wenye mvuto wa kisura na kimaumbile.

Kwa kifupi wanaume wamelalamikiwa na wanawake kwa tabia zao za kutoridhika na walivyonavyo, wakitamani kila wakionacho mbele yao, yaani kila mwanamke anayepita mbele yao hutamani ‘kumvua nguo’.

Lakini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, inadaiwa kuwa wanawake ndio wenye mapenzi ya kweli kiasi kwamba wanapowapenda wanaume huwapenda kweli kweli.

Lakini pia, wapo wanasisitiza kuwa wanaume ndio wenye mapenzi ya dhati kiasi kwamba wanapopenda hupenda kweli na si maigizo kama ilivyo kwa wanawake.

Ungana nami katika toleo la Jumanne ijayo ambapo nitakuletea ukweli juu ya mada hii kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa mambo ya mahusiano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -