Wednesday, October 28, 2020

NI KWELI WASICHANA WAZURI HAWAFAI KUOLEWA?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KARIBUNI wasomaji wangu katika safu hii inayowajia kila Jumanne na Jumamosi ikilenga kujuzana hili au lile kuhusiana na mambo ya kimapenzi.

Awali ya yote, nianze kwa kutoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba wa mmoja wa wasomaji wa safu hii ambaye ni mwanahabari za michezo na burudani, Amina Athuman, aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita visiwani Zanzibar akiwa kazini katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Amina ambaye ni mwandishi wa gazeti la Uhuru, alifariki dunia baada ya kupata kifafa cha mimba ambapo anatarajiwa kuzikwa leo mchana kwao Lushoto, mkoani Tanga.

Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, amina.

Baada ya salamu hizo za masikitiko, nigeukie mada ya leo ambayo inajaribu kujibu baadhi ya maswali au imani zilizopo ndani ya jamii.

Bila shaka utakuwa umeshawahi kusikia madai kuwa wasichana wazuri hawafai kuolewa na badala yake wanaume kushauriwa kuoa wasichana wa kawaida.

Unapowasikiliza wale wanaosisitiza hilo wanadai kuwa unapoona msichana mzuri ni sawa na kulima shamba la miwa karibu na shule, tena ile ya watoto wa walala hoi.

Wengine hudai kuwa kuoa msichana mzuri ni sawa na kufuga viranga katika eneo lililojaa mwewe.

Madai hayo yanatokana na imani yao kuwa mwanamume anapooa msichana mzuri anaweza kujikuta akiwa na presha muda wote kwani wanaume wengi watakuwa wakimtamani mwanamke wake huyo na hivyo kumtega kwa kila namna, iwe ni kwa kutumia fedha au vinginevyo.

Mwisho wa siku, msichana au mwanamke huyo anaweza kujikuta akishawishika na kutoka nje ya ndoa.

 

Ni kweli wasichana wazuri hawafai kuolewa?

Kabla ya kujibu swali hilo, tujiulize; hakuna wasichana wa kawaida ambao waliwahi kuwasaliti waume au wachumba zao?

Jibu la swali hili ni rahisi sana, unaweza kuangalia ni wanawake wangapi katika eneo unaloishi, sehemu yako ya kazi, ndugu au jamaa zako ambao ndoa zao zilivunjika kutokana na usaliti wa kimapenzi uliofanywa na mke au mchumba.

Kwamba wasichana au wanawake waliofanya hivyo walikuwa ni wazuri sana?

Wakati nikiwaachia ‘home work’ hiyo, ni vema tukakubaliana kuwa uhuni ni tabia ya mtu bila kujali kama ni mzuri au la.

Msichana au mwanamke anaweza kuisaliti ndoa yake kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kufuata mkumbo, tamaa, ulimbukeni, kulipiza kisasi, hulka na mengineyo kama hayo.

Juu ya kufuata mkumbo, wapo ambao wamekuwa wakishawishika kutoka nje ya ndoa baada ya kuona wenzao wanafanya hivyo, au kushawishiwa na ‘mashoga’ zao.

Lakini pia, wengine hujikuta wakiwasaliti waume au wapenzi wao kutokana na tamaa, wakiamini kwa kufanya hivyo wanaweza kupata fedha za kuwawezesha kumiliki vitu wasivyovipata kutoka kwa wenza wao.

Kwa upande mwingine, wapo malimbukeni ambao kumkataa mwanamume aliyemtongoza anadhani ataonekana mshamba, huku wengine wakifanya hivyo ili kulipiza kisasi baada ya kuhisi kusalitiwa na wapenzi au waume zao.

Lakini pia, wapo ambao kwao kuwa na mwanamume mmoja ni shida, hawa ni wale ambao wakati mwingine wamekuwa wakiitwa ‘wenye shetani wa ngono’ ambao hawawezi kukaa siku mbili bila kufanya tendo la ndoa na mwanamume hata kama si wake.

Pia, wapo wasichana au wanawake wengine wamekuwa wakijikuta wakitoka nje ya ndoa kutokana na mazingira yanayowazunguka… mathalani kazini kwa kushindwa kumkatalia bosi wake kwa hofu ya kupoteza kazi au kutoongezewa mshahara.

Kwa ujumla, kuna sababu nyingi zinazowafanya wasichana na wanawake kwa ujumla kuzisaliti ndoa zao bila kujali kama ni wazuri sana au la.

Kwa kuwa suala hili limekuwa likijadiliwa sana huko mitaani kwamba haifai kuona msichana mzuri sana kwa hofu ya kuibiwa, hebu niwakaribishe wasomaji wangu kila mmoja atoe maoni yake juu ya ukweli wa mada hii.

Maoni hayo nitayatoa katika toleo la Bingwa la Jumamosi hii. Ahsanteni sana na karibuni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -