Monday, November 30, 2020

Ni mwanamieleka yupi aliyetetea ubingwa wake kwa muda mrefu?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NEW YORK, Marekani

MPAKA sasa, mwanamieleka bora wa mwaka 2015, Kevin Owens ambaye anashikilia ubingwa wa Universal, anaonesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo lakini bado anakabiliwa na kibarua cha kuutetea ubingwa wake huo kama walivyowahi kufanya wanamieleka wengine.

Ni mwanamieleka yupi aliyewahi kushikilia mkanda kwa muda mrefu na ni mwanaume yupi wa shoka aliyetamba na ubingwa wa dunia kwa siku 4,040?

BRUNO SAMMARTINO – Siku 2,803

Ubingwa: Mei 17, 1963 dhidi ya Buddy Rogers

Alipoteza: Januari 18, 1971 dhidi ya Ivan Koloff

Katika pambano lililofanyika jijini New York, Marekani, Sammartino alitumia muda wa sekunde 48 tu kumtandika mpinzani wake, Rogers na kunyakua ubingwa wa dunia ambapo aliutetea kwa muda wa miaka saba, miezi nane na siku moja.

Sammartino alikuwa ni mpiganaji maarufu mno enzi hizo, mashabiki wake wangejazana kwenye ukumbi wa Madison Square kwa ajili ya kumshuhudia Mmarekani huyo mzaliwa wa Italia akizichapa na wanamieleka kama Waldo von Erich, Johnny Valentine, Ernie Ladd ‘The Big Cat’, Gorilla Monsoon na George Steele ‘The Animal’.

Mpinzani mkubwa wa Sammartino, alitambulika kama Killer Kowalski na alimtandika katika pambano lililofanyika kwenye ulingo wa Boston Red Sox Fenway Park.

Enzi hizo alikuwa ni mwamba usiotingishwa, lakini Waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha, mwaka 1971 alijikuta akitandikwa na Koloff kwenye ukumbi wa MSG na rasmi akavuliwa ubingwa.

BOB BACKLUND – Siku 2,135

Ubingwa: Februari 20, 1978 dhidi ya Billy Graham ‘Superstar’

Alipoteza: Desemba 26, 1983 dhidi ya The Iron Sheik

Katika muda wake wa kutetea ubingwa wake, Backlund alikutana na vikwazo kadha wa kadha. Kwa sasa anamnoa mwanamieleka, Darren Young.

Mkazi wa Minnesota, Marekani, Backlund alitandikwa na Antonio Inoki wa Japan katika pambano lililochezwa Novemba 1979, ingawa alifanikiwa kurudisha ubingwa wake wiki moja baadaye lakini watu wengi walidai kwamba ushindi huo ulikuwa batili.

Inoki aliamua kuchukua uamuzi wa kugomea ubingwa wa Backlund. Katika mpambano kati ya Backlund na Bobby Duncum, Mmarekani huyo alishinda tena mkanda wa pambano hilo na Shirikisho la Mieleka duniani (WWE), liligoma kumtambua Inoki kama bingwa mtetezi, Backlund ndiye aliyetambulika hivyo.

Kuanzia kipindi hicho cha kuanza kutambulika kama bingwa, Backlund alipambana na watu kama Harley Race, Ric Flair, Sgt Slaughter na Nick Bockwinkel, kabla ya kutandikwa rasmi na The Iron Sheik.

HULK HOGAN – Siku 1,474

Ubingwa: Januari 23, 1984 dhidi ya The Iron Sheik

Alipoteza: Februari 5, 1988 dhidi ya Andre The Giant

Zilikuwa ni siku 28 tu tangu Sheik ampokonye ubingwa Backlund na yeye akapokwa na mbabe wa zamani wa mieleka, Hulk Hogan.

Katika kipindi cha tambo za Hogan, Andre The Giant, alikuwa ni mpinzani wake maarufu. Mwaka 1987, Hogan aliendeleza ubabe kwa kushinda na kutetea mkanda wake wa WWE III, lakini alijikuta akiupoteza baada ya kuchapwa na Andre katika pambano lililopewa jina la ‘The Main Event’.

Katika maisha yake yote ya kupigana kwenye mieleka, Hogan alinyakua ubingwa wa dunia wa WWE mara sita ambapo ushindi unaokumbukwa zaidi ni ule dhidi ya Triple H kwenye pambano la ‘Backlash’ mwaka 2002 ambao aliutetea kwa jumla ya siku 2,185.

Ni Sammartino pekee ambaye amempiku Hogan kwa kutetea ubingwa wa dunia wa WWE kwa siku 4,040.

BRUNO SAMMARTINO – Siku 1,237

Ubingwa: Desemba 10, 1973 dhidi ya Stan Stasiak

Alipoteza: Aprili 30, 1977 dhidi ya Billy Graham ‘Superstar’

Rekodi hii ya Sammartino si kubwa kama ile ya mwanzo lakini kutetea ubingwa kwa siku 1,237 si mafanikio madogo pia.

Baada ya miaka mitatu tangu atandikwe na Koloff, gwiji huyo aliye hai alimtandika Stasiak ambaye naye alitoka kumchapa Pedro Morales na kunyakua ubingwa Desemba mosi mwaka huo 1973.

Sammartino alikutana na wapinzani wenzake wa muda mrefu wakiwemo Kowalski, Steel na Nikolai Volkoff, lakini pambano lake la kukumbukwa zaidi lilikuwa ni dhidi ya Stan Hansen ambalo alipambana akiwa mgonjwa wa shingo iliyovunjika, hata hivyo walisitishwa kupigana baada ya Sammartino kupoteza damu nyingi.

Katika pambano lingine baina ya Sammartino na Hansen, lilimalizika kwa Mmarekani huyo kuibuka mbabe lakini kadiri majeruhi yalivyokuwa yakimsumbua, alikuja kupigana na Billy Graham mwaka 1977.

PEDRO MORALES – Siku 1,027

Ubingwa: Februari 8, 1971 dhidi ya Ivan Koloff

Alipoteza: Desemba mosi, 1973 dhidi ya Stan Stasiak

Morales anatambulika kama mwanamieleka bora zaidi kuwahi kutokea Puerto Rico na si kwamba ni kwa sababu ya kutetea ubingwa wake wa dunia wa WWE kwa zaidi ya siku 1,000 lakini aliwahi pia kushinda taji la ‘Intercontinental’ zaidi ya washiriki waliowahi kuwania taji hilo na kulitetea kwa siku 619 akivuka zile za Don Muraco (541), The Honky Tonk Man (454) na Tito Santana (443).

Morales, mwanamieleka wa kwanza kunyakua mkanda wa WWE, ‘Intercontinental’ na ‘World Tag Team’, katika mapambano yake na Stasiak alikuwa akipata ushindi mzuri kabla ya kuupoteza kwenye pambano lao lingine lililopigwa Philadelphia, Marekani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -