Tuesday, November 24, 2020

NI MWENDO WA KULA BATA KWA SANA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA BEATRICE KAIZA,

INAKUWAJE  wadau  wa kipande hiki cha ‘Hapa Bata Tu’, kama kawaida kila ifikapo Ijumaa hadi Juma pili ni mwendo wa kula bata kwa sana.

BINGWA ipo kwa lengo la kutoa burudani na elimu kwa jamii.

Mashabiki na wapenzi wa kipande hiki twende sawa ili kujua ni viwanja gani vitakiwasha wikiendi hii.

HII KWA MAPOPO

Ni muda wako sasa wa kuonekana kijanja ukiwa na mikato ya aina yake, kwani wajanja wote tunakutana  maeneo fulani ya kijanja. Ili sote tukutane sehemu moja, soma hapo chini ili kujua nimekuandalia nini leo kwenye eneo hili, haya twende kazi.

Club Element (Masaki)

Ijumaa hadi Jumamosi ni disko muziki mnene na Dj Sinyolita.

Escape One (Mikocheni)

Kama wewe ni mdau wa Kareoke basi dondoka pande hii siku ya Ijumaa, maana itakuwa ni Karaoke Night, halafu Jumamosi tunapunga upepo na Skylight.

Maisha Basement (Makumbusho)

Ijumaa ni Wiggle Night na Dj Skad na Jumamosi ni Ibiza Night na Dj Ally B.

WAZEE WA BAND & TAARAB.

Dar Live (Mbagala)

Jumapili kutakuwa na Manchester Band.

Sikinde Ngoma ya ukae (Bendi)

Kwa wale vijana wa zamani pia hatujawaacha mbali wikiendi hii, Sikinde Jumamosi watakuwa Mwembeyanga (Temeke).

Jumapili watakuwa DDC Kariakoo (Old Trafford).

Twanga Pepeta

Wazee wa kutwaga na kupepeta Jumamosi hii watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani,

Jumamosi Mango Garden, Jumapili Toroka uje Kimara.

TABORA JAZZ STARS (SINZA)

Ijumaa ni usiku wa Segere Matata katika ukumbi wa BMM PUB, halafu Jumamosi ni usiku wa Heshima chini ya Ramadhani Kitenge.

WAKALI WAO (MODERN TAARAB)

Hapo sasa, kama nyonga ndiyo mpango mzima basi ibuka Travertine Hotel, Magomeni, Jumapili hii maana Wakali Wao watawarusha wale ndugu zetu wa vidole hewani.

WAZEE WA BAND

Safari Resort (Kimara)

Ijumaa hadi Jumapili kutakuwa na burudani itakayoporomoshwa na FM Academia.

MOVIES

MLIMANI CITY (SURVEY)

Hapa kutakuwa na movie kali na wajanja wote wa jiji wanakutana hapa, cha kufanya kamatia 3D yako ili kuweza kutizama kwa ukaribu.

Power Rangers, Life, Phullauri, Kong, Beauty and the Beast, Logan, Karibu Kiumeni.

Hizo ndizo movie ambazo zitakuwa hewani pande hizi za Mlimani City.

Imeandaliwa na Beatrice Kaiza, kama una kiwanja chako na unataka wadau wajue nini kinatokea maeneo yako, kamatia simu kisha tuma ratiba katika namba hii 0626 664 991 tu, usipige simu  maana hapa bata tu hainaga kuchagua.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -