Monday, August 10, 2020

NI SAMATTA AU MSUVA?

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA THERESIA GASPER

JAPO kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars kina wachezaji wengi wenye ubora, lakini mashabiki wamejikuta wakiwa njiapanda kuwa nani kati yao ndiye nguzo ya timu.

Na hilo limekuja baada ya Simon Msuva kuibuka kuwa shujaa wa timu hiyo katika mechi mbili mfululizo dhidi ya Botswana na Malawi wikiendi iliyopita.

Katika mechi hizo za kirafiki za kimataifa, Msuva alifunga mabao mawili dhidi ya Malawi katika ushindi wa mabao 2-0, kabla ya juzi kufunga walipotoka sare ya bao 1-1 na Malawi.

Awali, Mbwana Samatta anayekipiga Ubelgiji, ndiye aliyekuwa akionekana kuwa mhimili wa Stars, lakini kuibuka kwa Msuva anayecheza Morocco kunaonekana kuibua mjadala mpya.

Mathalani katika mchezo wa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, wachezaji hao walionekana kuibeba mno Stars, hasa Msuva ambaye alikuwa akimlisha mipira mwenzake huyo mara kwa mara japo alishindwa kuitumia.

Katika mchezo huo, Msuva ndiye aliyeonekana kuwa hatari zaidi kwa mabeki wa Malawi, kwani aliweza kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga mabao, lakini zilishindwa kutumiwa.

Ni makali yake hayo ndiyo yaliyoiwezesha Stars kuepuka kipigo cha nyumbani baada ya Msuva kufanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao la kusawazisha kutokana na mpira wa kona uliombabatiza beki wa Malawi na kujaa nyavuni.

Mwisho wa mchezo, mashabiki waliokuwa wamejikusanya nje ya uwanja huo, lakini pia katika vijiwe na vyombo vya usafiri, walibaki wakitafakari juu ya ubora wa Msuva dhidi ya Samatta, huku wakijiuliza nani anastahili kuitwa nguzo ya Taifa Stars kwa sasa?

Katika mabishano hayo, wengine walionekana kukiri kuwa Msuva wa sasa si yule aliyekuwa akiichezea Yanga kwani amebadilika kwa kiasi kikubwa kuonyesha jinsi kutua kwake nchini Morocco anakocheza soka la kulipwa, kulivyoboresha kiwango chake.

Lakini pia wapo wanaoamini ubora wa Msuva umechangiwa mno na Samatta ambaye amekuwa karibu mno na winga huyo, akimsisitizia kupambana ili mwisho wa siku naye aweze kupata timu Ulaya hali itakayoifanya Tanzania kuanza kutambulika barani humo kama ilivyo kwa nchi za Hispania, Ujerumani, Italia, Brazil, Ghana, Nigeria, Cameroon na nyinginezo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -