Saturday, October 31, 2020

NI WAKATI WA KUWA NA LIGI YA WANAWAKE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA LEONARD MANG’OHA

TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, imetwaa taji la ubingwa wa Cecafa kwa wanawake na kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza kunyakua taji hilo.

Katika michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza katika Jiji la Jinja nchini Uganda, ilihitimishwa juzi kwa fainali iliyozikutanisha Kenya na Kilimanjaro Queens ambapo Kili waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Hatua iliyofikiwa na vijana hao inapaswa kupongezwa na kila Mtanzania mpenda michezo kutokana na heshima ambayo wamelipa taifa katika medani ya soka la wanawake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Wanastahili pongezi kutokana na ukweli kwamba timu hiyo ilienda kwenye mashindano hayo huku ikiwa haina maandalizi yoyote ya maana hasa kwa kuwa mashindano yenyewe yalikuwa kama ya kushtukiza tu.

Hawakuwa na maandalizi kwa sababu hata jina lenyewe la timu baada ya ile Twiga Stars kuwa ya Taifa, jina la Kilimanjaro Stars lilipatikana  haraka haraka tu kutokana na ukweli kwamba mashindano ya kuishirikisha timu ya bara pekee hayakuwahi kufanyika.

Wachezaji wa timu hiyo ingawa wengi walikuwa kwenye timu ya Twiga Stars, walifanya juhudi binafsi kwa kushirikiana na walimu wao kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Taifa na kuleta heshima kwa taifa letu.

Kwa juhudi zilizoonyeshwa na Kili Queens, inaonekana wazi kuwa vijana hao wana ari kubwa ya kusakata kandanda tena kwa mafanikio makubwa.

Ikumbukwe kuwa Tanzania haina ligi ya soka la wanawake, hivyo wachezaji hao hutokea katika klabu za mitaani kabla ya wale wachache waliopata nafasi ya kuchukuliwa na timu za majeshi ili kusaidia kuvilinda vipaji vya wachezaji hao.

Kutokana na juhudi zilizoonyeshwa na timu hiyo, TFF na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa mchezo huo, sasa wafikirie upya namna ya kuanzisha ligi maalumu ya wanawake kwani hadi sasa licha ya Kampuni ya Proin Promotion kudaiwa inadhamini Ligi ya Wanawake, lakini hadi sasa hakuna ligi yoyote iliyofanyika.

Hivi karibuni Shirikisho la Soka nchini (TFF), lilitangaza kuanza kwa ligi ya soka kwa wanawake ikijumuisha timu kutoka sehemu mbalimbali na ninaamini kuanzishwa kwa ligi hiyo kutasaidia sana kupatikana kwa timu imara zaidi ambayo itaendeleza mafanikio haya ya Kili Queens katika anga za kimataifa.

Kwa kawaida katika mchezo wa soka timu inayopata nafasi ya kushiriki michuano mingi au inayocheza idadi kubwa ya mechi za kimashindano na zisizo za kimashindano, huwa katika ubora mzuri ukilinganisha na timu iliyocheza mechi chache.

Kwa mantiki hii ni wazi kuwa Kili Queens itakuwa katika nafasi bora zaidi ikiwa wachezaji wake watapata nafasi ya kushiriki michuano mingi ikiwamo ya ligi.

Kocha mwenye uzoefu mkubwa na soka la Tanzania, Adolfu Rishard, alielezea mtazamo wake kuhusiana na timu hiyo kutwaa taji la Cecafa kwa wanawake ambapo alisema amefurahishwa na kile kilichofanywa na timu hiyo kwani wako baadhi ya wachezaji na viongozi waliokuwepo katika timu iliyoshiriki michuano ya Afrika ambao walionyesha nia kubwa ya kutafuta mafanikio.

Alisema kuanzishwa kwa ligi ya wanawake kutasaidia kuboresha viwango vya wachezaji na pia ni vema zaidi kuanzishwa kwa mfumo mzuri wa kupatikana wachezaji kushika nafasi za wale walio na umri mkubwa.

“Kuna umuhimu wa kuwa na mahali patakaposaidia kupata vijana wengine chipukizi angalau kusaidia kuimarisha kikosi hicho. Tuna michuano ya Airtel Rising Star, lakini nadhani baada ya michuano hiyo lazima kuwe na mwendelezo wa mechi za wasichana ndiyo maana naona suala la kuwa na ligi ni muhimu sana,” alisema Rishard.

Anasema pia wanapaswa kupatikana walimu sahihi ili kuwezesha kuwaandaa wachezaji na anaishukuru sana TFF na Fifa kwa kuleta kozi ya makocha wanawake ili kuhakikisha kwamba kunakuwepo na makocha ambao wana weledi katika eneo hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -