Tuesday, November 24, 2020

NIDHAMU YA MCHEZO ILIAMUA MATOKEO SIMBA, YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HASSAN DAUDI

JUZI kulikuwa na vita kali ya mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara ‘Kariakoo derby’, uliowakutanisha mahasimu Simba na Yanga ambapo Wekundu wa Msimbazi waliibuka kidedea.

Mara nyingi watani hao wa jadi wanapovaana huwa ni burudani ya kutosha kwa mashabiki wa soka hapa nchini, ndivyo ilivyokuwa Jumamosi  iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kwa waliobahatika kuutazama mchezo huo aidha wakiwa kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kujaza takribani mashabiki 60,000, waliokaa kwenye viti  au kupitia vituo vya televisheni, watakiri kuwa haukuwa mtanange wa mchezo mchezo.

Binafsi naamini ilikuwa moja kati ya mechi bora kuwahi kuzikutanisha timu hizo kongwe katika historia ya soka la hapa nchini.

 

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kujizolea pointi zote tatu, matokeo yanayowafanya kubaki kileleni wakiwa wamefikisha pointi 54 dhidi ya 49 za Yanga wanaoshika nafasi ya pili.

Hata hivyo, juzi Yanga walikuwa na asilimia kubwa ya kushinda lakini hawakuwa na nidhamu ya mchezo na hilo ndilo lilosababisha wapoteze pambano hilo.

Kwanza, Yanga walipata bao la kuongoza mapema mno na pia Simba walicheza pungufu kwa muda mrefu, baada ya staa wao, Janvier Bokungu kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya tatu.

Kwa mantiki hiyo, Yanga walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda lakini hawakuwa na nidhamu ya mchezo, hivyo kuruhusu bao la kusawazisha kabla ya kugongwa msumari wa mwisho.

Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tano kupitia kwa Simon Msuva, baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Simba, Novatus Lufunga.

Kwa walioitazama mechi ile, watakubaliana na mimi kuwa Yanga waliridhika mara tu baada ya kupata bao hilo la penalti.

Wachezaji wa Yanga walitengeneza nafasi nyingi lakini tayari walionekana kuridhika na matokeo hayo ya bao 1-0.

Aina ya uchezaji wao haikuonyesha kuwa walihitaji kitu kingine zaidi ya filimbi ya mwisho kutoka kwa mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza.

Kwa maana nyingine, umakini na ufanisi wa safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji ulipotea ghafla, baada ya kuona wanaongoza, wakiamini mchezo ungemalizika kwa matokeo yale.

Kwa mfano; kitendo cha mlinda mlango, Deogratius Munish ‘Dida’ kulimwa kadi nyekundu kwa kuchelewesha mpira kiliashiria kuwa Yanga hawakutaka ushindi zaidi ya ule wa bao 1-0.

Kutokana na nidhamu ya mchezo hasa makosa ya wazi kwa washambuliaji, kitendo cha Bokungu kulimwa kadi nyekundu na kutolewa uwanjani, hakikuwa na faida yoyote kwa Yanga. Ni kama walizidi kujiamini na kucheza kwa kuridhika.

Kwa lugha ya rahisi, Yanga waliamini wamemaliza kazi, jambo ambalo ni baya hasa katika mchezo wa soka ambapo dakika 90 ndizo mwamuzi.

Yanga wakajikuta wanazidiwa nguvu kila muda ulivyokuwa ukizidi kwenda, huku Simba wakionekana kufufuka na kuanza kuutawala mchezo.

Kimsingi, Yanga waliipa kisogo nidhamu ya mchezo na ndicho kilichowaangusha na kujikuta wakipoteza pointi tatu ambazo walikuwa wameshaziweka mkononi.

Simba wanastahili pongezi kwa utulivu na nidhamu yao ya hali ya juu katika mchezo wa juzi. Waliuheshimu mchezo wa soka na hatimaye ukawazawadia kile ambacho wengi hawakukitarajia.

Baada ya kufanya uzembe na kuruhusu bao la mapema la mkwaju wa penalti, wachezaji wa Simba hawakuhamaki. Walitulia na kujipanga upya huku wakijilinda na kuepuka kufanya makosa mengine ambayo yangewagharimu.

Nilitegemea kuona Simba wakicheza kwa presha na hatimaye kufungwa bao jingine kwa muda mfupi baada ya lile la kwanza. Haikuwa hivyo.

Ilikuwa ngumu kuliona pengo la Bokungu uwanjani, ni kama ambavyo haikuwa rahisi kuamini Yanga walikuwa 11 na Wekundu hao wa Msimabzi wakiwa pungufu.

Kutokana na nidhamu kubwa waliyokuwa nayo wachezaji wa Simba, wakafanikiwa kuchomoa bao la kwanza katika dakika ya 66 kupitia kwa Laudit Mavugo.

Licha ya kuwa 10 uwanjani, tofauti na wenzao Yanga, Simba hawakuridhika na matokeo hayo ya sare ya bao 1-1 na badala yake waliendelea kulishambulia lango la wapinzani wao hao ambao tayari walishapotea uwanjani.

Nidhamu yao ya mchezo ilizaa matunda dakika 15 baadaye baada ya Shiza Ramadhani ‘Kichuya’ kufunga bao la pili na la ushindi kwa Wekundu wa Msimbazi.

Kutokana na uimara wa vikosi vyote viwili, ni wazi mchezo wa juzi haukuwa mwepesi kwa pande zote, yaani hakukuwa na timu iliyokwenda uwanjani na matokeo mfukoni.

Kilichoamua mtanange huo ulioteka hisia za mashabiki wengi wa soka ni nidhamu ya mchezo ambayo ni pamoja na kutoridhika na matokeo, kutumia vizuri nafasi unazopata na kuepuka makosa yanayoweza kuigharimu timu hasa kwenye safu ya ulinzi.

Kwa upande wa Yanga, nidhamu ya mchezo ilikuwa chini hasa baada ya bao lao la mapema na kutolewa uwanjani kwa Bokungu, lakini Simba walionyesha nidhamu ya hali ya juu ikiwamo kutokata tamaa licha ya kuongozwa mwanzoni kabisa mwa mchezo na kuwa pungufu uwanjani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -