Tuesday, November 24, 2020

NIKKI WA PILI: VITA DAWA ZA KULEVYA IENDE SAMBAMBA NA KUKUZA UCHUMI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA BEATRICE KAIZA,

KAMA ilivyo kawaida kila Jumanne Jiachie na Staa Wako huwa inamshusha staa mmoja wa nguvu kutoka ardhi ya Bongo kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali ya wapenzi wake.

Kama nilivyokuahidi wiki iliyopita, Jiachie na Staa Wako baada ya kumsaka kwa udi na uvumba hatimaye ilimpata  mkali wa hip hop wa kundi la Weusi, Nickson Simon, maarufu zaidi kwa jina la Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili kwa wakati huu anapeta na singo yake ya  ‘Sweet Mangi’, ambayo imezidi kumweka juu kwenye medani ya muziki wa Bongo fleva.

Kabla ya kusumbua na Sweet Mangi, Nikki, ambaye ni mdogo wa damu wa staa wa hip hop Joh Makini, ambaye pia anawakilisha kundi la Weusi, aliwahi kutamba na ngoma kama Baba Swalehe, Nje ya Box na Role Model.

Husika hapa chini, soma kwa makini ili kuweza kujua nini Nikki wa Pili amewajibu mashabiki zake, mambo yalikuwa kama ifuatavyo.

Swali: Gladyness Sanka, Kisongo Arusha. Umejipangaje kuhusu suala ya kuoa.

Jibu: Bado nipo nipo, unajua suala ya kuoa ni mipango, huwezi kukurupuka, unatakiwa kujipanga ili kuwa na familia bora.

Swali: Editha Emanuel wa Serengeti, unaipa ushauri gani jamii ya Kitanzania kuhusiana na vita dhidi ya dawa za kulevya.

Jibu:Tupo katika nchi yenye uchumi mdogo, hivyo kama serikali inataka kupambana na dawa za kulevya inabidi ikuze uchumi kwanza, katika nchi yoyote kama yetu lazima biashara hizi ziwepo ili watu waweze kujikimu mahitaji yao muhimu.

Swali: Pendo John wa Kimara, Dar es Salaam. Unaitumiaje mitandao ya kijamii.

Jibu: Mitandao ya kijamii naitumia kama sehemu ya kutoa elimu kwa jamii na kubadilishana mawazo na mashabiki wangu.

Pia naitumia kutangaza kazi zangu kwa mashabiki.

Swali: Koku wa Mwanza, unakutana na changamoto zipi katika kazi zako za sanaa.

Jibu: Nimepitia changamoto nyingi hadi kufikia hapa, kwa mfano miaka ya nyuma ilikuwa vigumu kujua nini mashabiki wanataka, kipi unatakiwa kufanya ili kwenda sambamba na soko.

Hapa nina maana kutoa kazi zenye ubora zaidi ambazo zitafanya vema ndani na nje ya nchi.

Pongezi: Mama Juma wa Moshi. Mimi ni shabiki wako namba moja, nakupongeza kwa uchapakazi wako, pia nakutakia mafanikio mema.

Jibu: Asante sana mama Juma.

Swali: Emmy wa Ilala, Dar es Salaam. Naomba kujua kutoka kwa Nikki wa Pili, amejipangaje kuwasaidia wasanii chipukizi ili na wao waweze kufanikiwa.

Jibu: Kuhusu kuwasaidia chipukizi, kwanza kabisa wao wenyewe wanatakiwa kutumia fursa walizonazo na kuwa wabunifu zaidi kwa kutumia elimu na vipaji walivyobarikiwa na Mungu, halafu mambo mengine yatafuata.

Swali: Bakari wa Dodoma, nje ya sanaa unajishughulisha na nini.

Jibu: Nje ya sanaa mimi ni mfanyabiashara.

Swali: Saidi Shaibu wa Kilimanjaro. Nikki mpaka sasa umefanikiwa kupata watoto wangapi.

Jibu: Bado sijafanikiwa kupata mtoto.

Pongezi: Mozes wa Kibaha, Dar es Salaam na Amiri Omary wa Morogoro. Kwenye sekta ya muziki wa hip hop Weusi mnafanya vizuri zaidi kuliko kundi lolote hapa nyumbani, hongereni kwa hilo.

Jibu: Asante sana tupo pamoja.

Swali: Phidelis Wella wa Magomeni, Dar es Salaam. Unawashauri nini wasanii wachanga ambao wanatamani kutimiza ndoto zao ili wafikie hatua uliyofikia wewe.

Jibu: Wasanii wanatakiwa kuwa na mbinu mpya ili kuleta kitu vipya kwa jamii na kuwa wabunifu zaidi ili kulisongesha soko letu liwe la kimataifa zaidi.

Pongezi: Antony Mselewa wa Kondoa. Hongera kaka Nikki kwa kazi nzuri, pia nakutakia kazi njema na mafanikio mema.

Jibu: Asante sana.

Ushauri: Loveness wa Morogoro, muziki umekuwa mgumu kwasababu ya wasanii kuongezeka, ushauri wangu kwako unatakiwa kuwa mbunifu kwa kutoa video nzuri ili kukimbizana na soko la sasa.

Pongezi: Mwasiti Omary wa Dar es Salaam. Napenda kazi zako, kwani wewe ni msanii unayejitambua na unajua nini unafanya kwenye tasnia ya muziki, nakuombea endelea na misimamo yako hiyo hiyo na kujiamini zaidi, Mungu akuzidishie.

Hawa ni baadhi ya mashabiki wa Nikki wa Pili waliojitokeza kumuuliza maswali na kumpa pongezi pamoja na ushauri.

Katika toleo lijalo tunamleta kwenu aliyekuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, ambaye pia ni msanii wa filamu kutoka kiwanda cha ‘Bongo Movies’.

Tumia fursa hii kumuuliza maswali ili kukata kiu yako, pia unaweza kumpa ushauri kwa kutuma sms kupitia namba ya simu iliyoko hapo juu, majibu yatapatikana hapa hapa katika toleo la Jumanne ya wiki ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -