Wednesday, January 20, 2021

NILISHAKUFA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia

Nilikaa kwenye kochi na kujiuliza kama Paulina alikuwa akitumia kiasi cha shilingi 7,000 hadi 12,000 kwa matumizi tu ya urembo na mambo yake mengine, je, leo nikimwambia kuwa nimefukuzwa kazi atanielewa?

Nikiwa nimejiinamia pale kwenye kochi, Paulina alitoka chumbani.

 “Heee! Mume wangu umerudi saa ngapi,” aliuliza kwa mshangao.

Niliinua macho kumtazama, hakika alikuwa amependeza sana.

SASA ENDELEA

“Sasa hivi ndio naingia,” nilimjibu kwa unyonge mkubwa.

“Vipi kuna tatizo, halafu mbona leo umewahi kurudi kiasi hiki, saizi ni saa sita,” aliniuliza huku akinijia pale nilipokuwa nimekaa.

Alipofika alikaa karibu yangu na kuniwekea mkono kwenye bega langu. Alinitazama kwa macho yake mazuri huku harufu nzuri ya marashi yake ikizidi kunipa wakati mgumu wa kujieleza.

“Mume wangu kuna nini, mbona u mnyonge kiasi hicho?” aliniuliza kwa sauti nyororo.

“Nimefukuzwa kazi,” nilimjibu kwa ujasiri sikuona haja ya kuficha ficha.

“Eti niniii!?”

Paulina alishtuka hadi moyo wangu ukaumia.

“Nimefukuzwa kazi,” nilirudia kauli yangu.

“Kivipi! Sikuelewi, umefukuzwa kazi, umeanza utani wako?” aliniuliza akionekana kuchanganyikiwa.

“Sina tena kazi nielewe hivyo mke wangu.”

“Fredy unanidanganya sio? Au umeona pesa unazonipa mwisho wa mwezi ni nyingi hadi ukafikia hatua ya kutunga uongo?” aliuliza Paulina akiwa na ndita mbili usoni.

“Siwezi kukuongopea mke wangu. Kuna mtu kule kazini kapeleka mashtaka ya uongo kwamba  nilikuwa natoa bidhaa nje ya kiwanda kwa magendo.”

Paulina aliposikia hivyo alishusha pumzi, akauweka mkoba wake mezani. Hakuwa na hamu tena ya kuuvaa kwa ajili ya kutoka. Alinigeukia na kunitazama macho yake malegevu yaliondoka na kubaki macho ya kawaida.  Nilianza kuogopa maana alibadilika ghafla. Alinitazama sana kisha baadaye akaniambia.

“Sawa, lakini fanya juu chini upate kazi nyingine, tena haraka iwezekanavyo. La sivyo, nitarudi kwetu maana sitaweza kufa na njaa huku nikijiona.”

Sikuyaamini maneno yake, nilidhani ni utani. Nikamtazama kwa sura ya kujichekesha na kumuuliza.

“Mke wangu unaweza kuchukua uamuzi huo?”

“Fredy huu si wakati wa utani. Umeniambia na wewe hutanii na mimi sitanii. Unafikiri nitaishije humu ndani bila chakula wala nguo nzuri. Nakupenda Fredy, lakini siwezi kuvumilia njaa, nakupa mwezi mmoja uwe umetafuta kazi bila hivyo utakuja kunichukua kwetu, tumeelewana?” aliongea Paulina akiwa amebadilika sana.

Nilipotaka kuongea jambo, alichukua mkoba wake na kuondoka.

“Paulina mke wangu unakwenda wapi, njoo tujadili basi,” niliongea kwa huruma.

Kabla hajafika mlangoni, alinigeukia na kuniambia.

“Ninatoka kidogo nikirudi nikute umeshaanza kufikiria nini cha kufanya, sawa?”

Baada ya kusema hivyo, alitoka na kuniacha pale sebuleni nikiwa nimezubaa mtihili ya mtu aliyenyeshewa na mvua kubwa. Nilihema kwa nguvu na kuyatafakari maneno yake kwa haraka sana. Nguvu zilizidi kuniishia, maana sikutegemea kama mke wangu atazungumza yale maneno. Ingawa mwanzoni nilikuwa nikihofia kuwa ataipokea vibaya taarifa yangu ya kufukuzwa kazi.

Baadaye nilitoka nyumbani na kwenda kwa rafiki yangu Halid. Nilimsimulia kila kitu kuhusu kufukuzwa kazi.

“Pole sana besti yafaa ujipe moyo, kwani huu ndio mtihani wako mkubwa katika maisha yako, ukiushinda, utakuwa umepiga hatua kubwa sana,” aliongea Halid akinifariji.

“Asante sana ila sijui nianzie wapi kutafuta kazi nyingine, yaani nimechanganyikiwa Halid,” niliongea nikimtazama Halid usoni.

“Nakushauri anza kutafuta kwenye viwanda vingine vya nguo na kuwaeleza umefanya kazi wapi ili iwe rahisi wao kukuajiri.”

Halid alinishauri mengi sana, akaniahidi kunisaidia kwa kunitafutia kazi. Lakini katika maongezi yangu, sikumwambia kuhusu alichoniambia Paulina. Nilijikuta naficha kila kitu ambacho mke wangu ananiambia.

Hata mama sikuwahi kumwabia jambo lolote la Paulina nililokuwa nikiamini kuwa lingeweza kuleta mvurugano na kusababisha ndoa yangu kuyumba.

Baada ya kupokea mengi kutoka kwa besti yangu Halid, nilimuaga na kurudi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilikuta chakula mezani. Wakati huo Paulina alikuwa chumbani, nilijua atakuwa ameingia tu mara moja, kwani kwa wakati huo, ilikuwa ni saa moja kasoro jioni.

Nilikaa pale sebuleni na kuwasha runinga. Taarifa ya habari ilikuwa ikisomwa kwa wakati huo. Mtangazaji kituo cha Kaisavuna TV alikuwa akitangaza habari kutoka nchini Uganda. Alisema Serikali ya Idi Amin inaendelea kufanya maamuzi magumu juu ya uendeshaji wa taifa hilo katika sekta zote za kiuchumi.

Alisema baadhi ya viongozi waliokuwa wakimpinga kiongozi Idi Amin walikuwa wakipelekwa magerezani na baadhi yao kuhukumiwa kifo. Serikali ya kiongozi huyo, ilikuwa ikitaifisha baadhi ya mali za raia wake ili kufidia madeni ya Serikali na kukuza uchumi pamoja na nguvu ya kijeshi.

Niliendelea kusikiliza taarifa hiyo huku nikimsubiri Paulina atoke chumbani. Nilimsubiria kwa muda kidogo lakini hakutoka. Niliamua kunyanyuka na kwenda chumbani ambako nilimkuta akiwa amelala.  Alikuwa amelala kihasara nusu nzima ya mwili wake ilikuwa wazi, alijifunika sehemu ndogo ya shuka.

Hisia kali za mapenzi zilinikumbuka, mate yalitoka, nilitamani kuanzisha mechi ya kitandani muda huo huo. Lakini hata hivyo, ilikuwa si kawaida ya Paulina kulala muda huo. Ilibidi nimsogelee na kumuamsha.

“Mke wangu!,” Nilimuita huku nikimgusa begani.

Alizinduka usingizini na kunitazama.

“Mbona umelala mapema, twende tukale basi,” niliongea mimi kwa tabasamu la woga.

Sikuwa huru kwa muda huo kama siku zote maana nilikuwa ni mwanaume nisiye na kazi yoyote.

“Mimi nilishakula,” alinijibu Paulina na kulala tena.

Nilipatwa na mshangao, maana haijawahi kutokea mimi nikakaa mezani na kula chakula cha jioni peke yangu bila yeye. Mara nyingi alikuwa akipika, hunisubiria hadi pale nitakaporudi. Nikirudi tulikuwa tunakaa mezani wote na kula chakula pamoja kwa furaha zote.

Sikutaka kumuamsha tena, nilibaki na mshangao wangu nikiujiuliza kuwa labda alikuwa amechoka. Nilitoka chumbani na kurudi sebuleni na kukaa mezani. Nilifunua chakula na kuanza kula. Siku hiyo alikuwa amepika wali na nyama. Lakini chakula hakikuwa kitamu sana kama siku zote. Nilianza kujawa na wasiwasi fulani.

Baada ya kula nilizima runinga na kuelekea chumbani. Niliporudi nilimkuta akiwa amelala kihasara zaidi. Nilikumbuka kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya ratiba yetu ya mechi. Kwani tulikuwa na mechi hiyo kila Jumanne Jumamosi na Jumapili. Hata hivyo, ni wiki mbili tulikuwa tumepumzika kucheza mechi hiyo ambayo huwa inanifanya nijione paradiso kutokana na utundu wa hali ya juu, ambao huwa anauonyesha mrembo Paulina mke wangu wa ndoa.

Nilivua suruali yangu na kuvaa taulo. Nilipanda kitandani na kulala. Baadaye kidogo nilimtazama Paulina kwa jinsi alivyokuwa amebakiza mwili mzima nje ya shuka. Nilimeza mate huku hisia kali za mahaba zikianza kunitesa. Viungo vyangu viliwaka moto vikihitaji kutulizwa na penzi la mke wangu Paulina.

Lakini wakati mimi nikiwa katika mateso hayo, Paulina alikuwa akikoroma kwa usingizi mzito asijue chochote kuhusu mimi kwamba nilikuwa kwenye hali mbaya. Taratibu na kwa woga mkubwa nilianza kuupeleka mkono wangu kuelekea kwenye paja lake.

Niliogapa sana maana nilikosa amani. Hii ilitokana na kufukuzwa kazi huku nikiyaona mabadiliko madogo kutoka kwa Paulina. Nililigusa paja lake na baadaye kulishika. Paulina alitikisika kidogo na kujigeuza. Nilisita na kurudisha mkono. Wakati huo hisia kali za mapenzi zikiendelea kunisumbua zikihitaji mechi kali usiku huo.

Baadaye nilishindwa kuuhimili. Nilijivuta taratibu na kumsogelea kabisa. Nilimshika na kuanza kumpapasa. Alishtuka kutoka usingizi na kunitazama. Alinitazama kwa muda kidogo kisha akageukia upande wa pili.

Niliingiwa na wasiwasi na kuamua kumshika na kumpapasa tena ili kumkumbusha kuwa nilikuwa nikihitaji mechi usiku huo. Alishtuka tena na kunigeukia.

“Naomba ulale,” aliniambia na kugeuka kule kule.

Nilimshika tena na kumpapasa hadi karibu na goli lake, aligeuka haraka na kuniambia.

“Sijisikii, nimechoka usiku mwema,” aliongea kwa ukali kidogo.

Nilitulia kwa muda wa dakika 15 nikiendelea kuhangaika mwenyewe. Hisia za mahaba ziliendelea kunitesa vilivyo niliumia sana kiasi cha kutaka kulia. Mishipa ya nguzo yangu muhimu ilikakamaa ikishindwa kusinyaa. Niliteseka sana. Baadaye niliamua kumsogelea tena na kumshika, safari hii niliupeleka mdomo wangu katika mabega yake ili nijaribu kuamsha hisia zake. Lakini alishtuka kwa nguvu na kunigeukia.

“Hivi Fredy wewe sio mwelewa? Nimekwambia nimechoka, niache nilale,” aliongea kwa ukali zaidi ya mwanzo.

Nini kitaendelea? Usikose kesho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -