Tuesday, October 20, 2020

Nini kilichowapunguza kasi Leicester?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England

Nini kilichowamaliza mabingwa wa Ligi Kuu England wa msimu uliopita wa 2015–16? Kasi yao ya msimu uliopita ilikuwa ni moto wa kifuu?

Bila shaka hayo ndiyo maswali yaliyobaki vichwani mwa mashabiki wa soka hususani wale wa Ligi Kuu England.

Itakumbukwa kuwa, katika kile kilichowashangaza wengi, Leicester walinyakua ubingwa huo mbele ya klabu vigogo zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa hapo mwanzoni.

Ikipambana na Manchester United, Manchester City, Chelsea, Arsenal, Tottenham, Leicester ilitangazwa kuwa mabingwa.

Leicester walitangazwa kuwa mabingwa na hiyo ilikuwa ni mara yao ya kwanza katika historia ya timu hiyo.

Lakini tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016-17, mabingwa hao watetezi wamekuwa na mwenendo wa kusuasua.

Vijana hao wa Muitalia Claudio Ranieri, wameshinda mechi mbili pekee licha ya ligi kushuka dimbani mara saba.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka wanaamini kuwa mafanikio ya Leicester msimu uliopita yalitokana na ubovu wa klabu vigogo.

Wengi wanaamini kuwa kuimarika kwa wapinzani wao msimu huu, ndiyo kumesababisha Leicester kupoteza ramani.

“Ni kweli kuwa timu nyingine zinaogopa style yetu ya mashambulizi ya kushtukiza na ndiyo maana wanatuzuia kufanya hivyo,” alisema kocha Ranieri alipokuwa akizungumzia kuyumba kwa timu yake hiyo.

Inaelezwa huenda ushiriki wa Leicester katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ukawa umeivuruga kiakili Leicester, ikizingatiwa kuwa hii ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo.

Katika michuano hiyo, Leicester wameanza vizuri baada ya kushinda michezo  miwili dhidi ya Brugge na Porto.

Mfano, walipocheza na Liverpool, walipokea kichapo cha mabao 4-1 kabla ya matokeo hayo kujitokeza tena walipovaana na Manchester United.

Licha ya staa Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow, ni wazi straika huyo anahitaji muda kuwa katika kiwango bora alichokuwa nacho Urusi.

Bado hajaonekana kuzoea mazingira ya soka la England.

Mbali na Islam Slimani ambaye ameanza vizuri, bado Leicester inahitaji nguvu ya Mussa katika safu ya ushambuliaji.

Msimu uliopita, siri ya mafanikio ya Leicester ilikuwa ni mfumo wa ‘counter-attack’, ambapo Jamie Vardy alikuwa kiini cha safu ya ushambuliaji.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Muingereza huyo amekuwa akicheza chini ya kiwango, hivyo Mnigeria Musa anabaki kuwa sehemu muhimu ya safu ya ushambuliaji.

Lakini pia, kumiliki mpira ilikuwa ni moja ya sifa za Leicester msimu uliopita lakini msimu huu wameonekana wachovu katika hilo.

Kushuka kwa morali ya wachezaji ni sababu nyingine ya Leicester kushindwa kufanya vizuri msimu huu.

Morali ya ushindi kwa wachezaji wa leicester imeonekana kushuka kwa kiwango kikubvwa.

Katika mchezo wa soka, kushinda zaidi ya mara moja ni jambo gumu na changamoto kubwa ni kuwafanya wachezaji bora kuongeza kasi na kuwa bora zaidi.

Kwa Leicester, hilo halionekani kuwa na nafasi kubwa.

Badala yake, mzuka wa timu umepungua huku mastaa waliokuwa roho ya timu wakionekana kupwaya.

Mbali na hilo, hata historia ya Ligi Kuu England inaweza kuwa sababu ya Leicester kupotea.

Iko wazi kuwa, timu ya mwisho kutetea ubingwa wa ligi hiyo, yaani kuchukua mara mbili mfululizo, ilikuwa ni Man United na hiyo ilikuwa ni katika msimu wa 2008-09.

Si Man City wala Arsenal zilizoweza kutetea ubingwa au kukaribia kufanya hivyo.

Ni kipindi hicho ndipo Man United walikuwa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati huo, Man United walikuwa chini ya kocha Mskochi, Sir Alex Ferguson, huku wakiwa na mkali Cristiano Ronaldo.

Kwa mantiki hiyo, haitoshangaza kuwaona Leicester wakihaha msimu mmoja baada ya kuchukua ubingwa.

Ukiangalia vizuri, unaweza kugundua kuwa hata kikosi cha Leicester cha sasa kina mapungufu tofauti na kile cha msimu wa 2015-16.

Kuondoka kwa N’Golo Kante kumeidhohofisha kwa kiasi kikubwa safu ya kiungo ya Foxes.

Kante ametimkia Chelsea na pengo lake pale Leicester limeonekana wazi katika michezo yote saba.

Almanusura Riyard Mahrez na Vardy nao waondoke klabuni hapo kama si uimara wa kocha Ranieri.

Pasi za uhakika, uwezo wa kupandisha na kuzuia mashambulizi na mashuti makali ni miongoni mwa sifa kubwa alizonazo Kante ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa na manufaa kwa Leicester msimu uliopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -