Monday, October 26, 2020

NINI KINAENDELEA KATI YA BARCA NA MESSI?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

BARCELONA, Hispania

KWANINI Lionel Messi hajaongeza mkataba mpaka leo? Ni kweli anataka kuondoka Camp Nou kupata changamoto mpya? Na kama akiondoka, Manchester City ni klabu sahihi kwake?

Haya ni maswali yanayopasua sana vichwa vya wapenzi wa soka duniani juu ya ishu ya Lionel Messi.

Taarifa zinasema kuwa yuko kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barcelona lakini bado kuna vipengele hawajakubaliana ndio maana kuna kuchelewa, lakini uvumi wa kujiunga na City umezidi kushika kasi, umeshawahi kujiuliza kwanini Messi hajawahi kukanusha taarifa hizi?

Kwa mujibu wa mwandishi wa The Sun, Antony Kastrinakis, awali Messi aligoma kusaini mkataba mpya mpaka hasimu wake Cristiano Ronaldo atakaposaini mkataba na Real Madrid, unajua kwanini?

Messi alihitaji kujua kwanza Ronaldo atalipwa kiasi gani kwenye mkataba wake na hili tayari amefanikiwa.

Tayari Ronaldo ameshaini mkataba wa miaka mitano zaidi utakaomwingizia pauni milioni 45 kwa mwaka na taarifa zinadai kuwa Messi ameuambia uongozi wa Barca kuwa anataka kulipwa pauni milioni 55 kwa mwaka, jambo linaloonekana kuwapa kigugumizi viongozi wa klabu hiyo.

Kastrinakis anaamini dau la Ronaldo limetumika kama kipimo kwa uongozi wa Messi, ili kumfanya nyota huyu wa kimataifa wa Argentina kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani.

Na katika kulishikiniza hilo, Messi ameamua kuitumia Man City kama kigezo cha kuisukuma Barca kumpatia dau hilo.

Lakini kwa upande wa mabosi wa City wao wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutaka kumsajili Messi kwa gharama yoyote ile duniani ili kumuunganisha tena nyota huyo na kocha wao, Pep Guardiola.

Mkataba wa sasa wa Messi na Barca unamalizika mwaka 2018, hivyo kwa namna yoyote ile lazima uongozi wa mabingwa hao wa La Liga utakuwa kwenye mpango wa kutaka kumwongeza Leo mkataba mpya mapema.

Ikumbukwe kuwa tangu Messi alipoanza kuichezea Barca mwaka 2004, ameipa mafanikio mengi klabu hiyo na kujitengenezea heshima kwenye mioyo ya mashabiki wao.

Licha ya kutwaa mataji nane ya La Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Messi ni balozi mkubwa wa kuzitangaza biashara za klabu hiyo kwenye ulimwengu wa wapenda soka.

Kumpoteza Messi kutakuwa ni sawa na kupoteza nembo ya biashara ya klabu, hivyo si jambo linaloweza kufanywa kirahisi na viongozi wa Barca.

Ndiye mfungaji bora wa klabu hiyo, amevunja na kutengeneza rekodi nyingi ndani na nje ya Barca, sifa hizi pekee zinatosha kumfanya awe na jeuri katika suala hili la kusaini mkataba mpya.

Huenda kweli City wana nia ya kutaka kumsajili Messi, lakini ukweli uliowazi ni kuwa Leo mwenyewe hana mawazo ya kujiunga na matajiri hao wa jiji la Manchester kwa wakati huu.

Tena ukizingatia hasimu wake Ronaldo ameamua kusalia kwa miaka mingine mitano nchini Hispania, bila shaka mawazo ya Messi ni kutaka kuendelea kuitumikia zaidi Barca.

“Sote tunaridhishwa na uwezo wake, hata Leo anafurahia mazingira ya klabu, tulishakubaliana kuwa atamaliza maisha yake ya soka akiwa hapa,” aliwahi kunukuliwa Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu.

“Bodi yote tumekubaliana kuwa Messi atabaki hapa na tunaamini uwepo wake utachangia mafanikio makubwa zaidi ya aliyotupatia awali.”

Akiwa City, Messi anaweza kulipwa vizuri, kucheza anavyojisikia, kuwa mfalme wa klabu lakini daima hataweza kuipata heshima aliyoipata akiwa Barca.

Kimsingi Messi anataka kuendelea kubaki Barcelona ila anachokifanya hivi sasa ni kuchanga vyema karata zake ili kupata mkataba mnono, hizi habari za City zitabaki kuwa uvumi tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -