Sunday, January 17, 2021

Niyonzima afurahiswa na Pluijm

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HUSSEIN OMAR

WAKATI mashabiki wa Yanga wakiduwazwa na kiwango cha juu alichokionyesha  mchezaji, Haruna Niyonzima, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Toto Africans, kiungo huyo amefunguka na kusema anafurahia zaidi  uamuzi wa kocha wake, Hans Van Der Pluijm wa kumpanga kucheza kiungo wa kati (namba nane) kuliko akicheza  winga.

Akizungumza na BINGWA jana, Niyonzima alisema anakuwa huru uwanjani akicheza nafasi hiyo kutokana na ukweli kwamba inamuweka katika nafasi nzuri zaidi ya kusambaza mipira kwa wakati na kuiunganisha timu.

“Unajua mimi napenda sana kucheza katikati ila kwa sababu kocha ndio bosi wa kila kitu, sina budi kumsikiliza lakini nimefurahi sana alipoamua kunipanga sehemu ambayo nimeicheza kwa miaka mingi,” alisema Niyonzima.

Alisema hapendi kuingilia masuala ya kiufundi ya benchi la ufundi la timu hiyo na kulazimisha apangwe nafasi hiyo, isipokuwa ameamua kiroho safi kucheza nafasi yoyote atakayopangwa uwanjani.

Kiungo huyo wa kutumainiwa wa Yanga na timu ya Taifa ya Rwanda, juzi alionyesha kiwango kikubwa katika mchezo dhidi ya Toto na kuwafanya mashabiki kumfurahia.

Niyonzima aliripotiwa kuwa na mgogoro na kocha wake Pluijm, kutokana na madai ya kushuka kiwango ambapo inaelezwa kwamba Pluijm alimtaka nyota huyo kukuza kiwango chake, la sivyo angeendela kukalia benchi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -