Wednesday, October 28, 2020

NIYONZIMA AMKATAA CLETUS CHAMA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU


KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima, amewaomba mashabiki wa timu hiyo nchini kutomlinganisha na Cletus Chama, ambaye ni kiungo mpya machachari wa timu hiyo mwenye udambwidambwi.

Chama alisajiliwa na Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, akitokea Lusaka Dyanamos ya Zambia, akiwa ni pendekezo la Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma.

Akizungumza na BINGWA jana, Niyonzima alisema anawaomba Watanzania, hasa wapenzi wa Simba, kuacha kumfananisha na Chama, kwani wao ni wachezaji wawili tofauti, japo wanacheza nafasi moja.

Alisema wote wawili wana uwezo mzuri, lakini yeye ni mchezaji ambaye anajiamini kuliko mchezaji mwingine na anapopata nafasi ya kucheza huwa hapendi masihara, hivyo ni suala la kujifua na mwalimu mwenyewe kujua ni mchezaji yupi anahitaji kumtumia kwa wakati huo.

“Msinifananishe na Chama, sisi sote ni wachezaji, mimi pia ni mchezaji mwenye vitu vyangu muhimu katika timu, siwezi kuhofia nafasi yangu, kwa sababu kucheza au kutocheza ni maamuzi ya kocha, ataona nani anafaa kwa wakati maalumu,” alisema.

Kiungo huyo Mnyarwanda aliongeza kuwa, yeye ni mchezaji wa Simba na hakuna timu ambayo inamhitaji, hata kama ipo ni lazima kufuata sheria za timu ambayo ina mmiliki.

Niyonzima aliongeza kuwa, tatizo kubwa na uongozi wake lilikuwa ni kuchelewa kwake kujiunga na timu, kama ambavyo walikuwa wamekubaliana na hakuna lingine zaidi ya hilo, lakini tayari wameshayazungumza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -