Friday, November 27, 2020

NIYONZIMA AMSHANGAA HAJI MWINYI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MAREGES NYAMAKA,

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, ameonekana kumshangaa nyota mwenzake, Haji Mwinyi, akidai kuwa iweje hadi leo anacheza soka nchini Tanzania, wakati umbo lake na uwezo vinamruhusu.

Akizungmza na BINGWA juzi, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Azam FC, ambao Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Obrey Chirwa, Niyonzima alisema Mwinyi ni miongoni mwa wachezaji wenye umbo zuri wanaopaswa kucheza nje ya Tanzania.

“Unajua Mwinyi ana umbo sana la kimpira, natamani ningekuwa mimi nadhani nisingekuwa hapa, katika soka la hivi sasa  watu wenye  mwili kama beki wetu huyo ni rahisi kupata nafasi endapo uwezo upo juu, sasa vyote Mwinji anavyo,” alisema Niyonzima.

Katika hatua nyingine, akizungumzia mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger ya nchini Algeria, Niyonzima alisema mashabiki wao hawapaswi kuogopa chochote, kwani wanao uwezo mkubwa wa kuwatoa nishai Waarabu hao.

“Binafsi nadhani tunaweza kuwafunga wapinzani wetu hao, kwani kwa sasa tupo vizuri kila idara, kilichopo mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi na badala yake watusapoti, kwani msimu huu tumedhamiria kufika mbali,” alisema.

Yanga watacheza na MC Alger mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, mchezo wa kwanza kabla ya kurudiana ugenini wiki ijayo ambapo Niyonzima anasema lazima wawaadabishe wapinzani wao hao.

Yanga wamelazimika kucheza michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa michuano ya Klabu Bingwa Afrika na sasa wenyewe wanadhani kuwa huu ni muda muafaka kupiga hatua kubwa, tofauti na msimu uliopita.

Tayari Kocha Mkuu wa kikosi hicho, George Lwandamina, alishaweka wazi mipango yake akidai kuwa, anachotaka kukifanya ni kuhakikisha timu yake inafika mbali kimataifa, kwani uwezo wa kufanya hivyo wanao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -