Sunday, November 29, 2020

NIYONZIMA AMTABIRIA LWANDAMINA MAFANIKIO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR


NAHODHA wa Yanga, Haruna Niyonzima, amemmwagia sifa kocha George Lwandamina, akisema anaweza kuipa timu hiyo mafanikio makubwa endapo atapewa muda.

Akizungumza na BINGWA jana, Niyonzima alisema Lwandamina ni kocha wa kipekee katika soka kwa ukanda huu wa Afrika na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kocha huyo anaijenga timu.

Alisema Lwandamina ni bora katika mbinu za kisasa, ni mtu ambaye ana vitu vya kipekee na anayejua nini anachokifanya tofauti na watu wanavyomchukulia.

“Naweza kusema ni moja kati ya makocha bora niliowahi kufanya nao kazi, ana kitu cha kufanya Yanga tumpe muda aweze kuzoea mazingira ya kazi na ligi yetu, atatupa mafanikio na kutupeleka mbali sana,” alisema Niyonzima.

Kiungo huyo alisema ni mapema kwa mashabiki wa Yanga kuanza kumuona Lwandamina hafai baada ya kushindwa kuipa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

“Mpira ni mchezo wa matokeo, tumefungwa na Azam FC bao 4-0 tukafungwa na Simba kwa penalti 4-2, huwezi kusema kocha hafai ukizingatia ndio kwanza ameanza kuijenga timu,” aliongeza Niyonzima.

Pia nahodha huyo alizungumzia utofauti kati ya Lwandamina na kocha wao wa zamani, Hans van der Pluijm, ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, akisema kila mmoja ana ubora wake.

“Kila mmoja ana mbinu na ufundi wake, cha msingi ni kumpa muda Lwandamina kwa kuwa ana kitu cha kuifanyia Yanga.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -