Friday, January 15, 2021

NIYONZIMA ATAENDELEZA KISMATI CHAKE SIMBA?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO wa Rwanda, Haruna Niyonzima, ni mmoja wa wachezaji wenye bahati kubwa ya kunyakua mataji mengi kwenye timu wanazozichezea. Ambapo mpaka sasa kwenye maisha yake ya soka amekwishanyakua jumla ya mataji 20.

Nyota huyo aliyezaliwa eneo la Gisenyi nchini Rwanda, alianza soka lake kwenye timu ya Etincelles, kisha Rayon Sports, APR kisha kutua Yanga na sasa amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Niyonzima ameichezea Etincelles mwaka mmoja (2005), kisha akakipiga Rayon Sports msimu wa 2006–2007 na kutimkia APR, ambako alicheza misimu mitano kuanzia 2007–2011 na kunyakua mataji manne ya Ligi Kuu Rwanda msimu wa 2007, 2009, 2010 na 2011.

Mataji mengine aliyonyakua akiwa APR ni Kombe la Rwanda ambapo amefanikiwa kubeba mataji manne msimu wa 2007, 2008, 2010 na 2011, huku mwaka 2007 na 2010 akiisaidia timu hiyo kunyakua mataji mawili ya Kombe la Kagame (Cecafa Clubs Cup).

Baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa APR, Yanga walivutiwa na nyota huyo na kumsajili mwaka 2011 na kusaidia klabu hiyo ya Jangwani kutwaa mataji tisa, yakiwamo manne ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Ngao ya Jamii mara tatu, taji moja la Kombe la Shirikisho Tanzania na Kombe la Kagame mara moja.

Katika msimu wake wa kwanza alipojiunga na Yanga (2011/2012) hawakufanikiwa kunyakua taji lolote na kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 49 na Simba kunyakua taji lao kwa mara ya mwisho kwa pointi 62, lakini msimu uliofuata 2012/13, walifanikiwa kunyakua taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa jumla ya pointi 60, huku Azam wakishika nafasi ya pili na Simba ya tatu.

Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013/14 taji lilikwenda Azam baada ya kujikusanyia pointi 62, Yanga walishika nafasi ya pili, kisha msimu uliofuata wa 2014/15, Yanga walinyakua tena taji hilo kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu.

Msimu wa 2015/16, Yanga walitetea taji lao kwa kukusanya pointi 73 na msimu uliopita walibeba taji la tatu mfululizo na la nne la Ligi Kuu kwa Niyonzima tangu atue Yanga, baada ya kujikusanyia pointi 68 sawa na Simba lakini wakatawazwa mabingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga.

Ukiachana na mataji hayo manne ya Ligi Kuu kwa Niyonzima tangu ametua Yanga, amenyakua mataji mengine kama Kombe la Kagame mwaka 2012/2013 wakiwa chini ya kocha wa Ubelgiji, Tom Saintfiet, baada ya kuwafunga Azam FC mabao 2-0 ambayo yaliwekwa nyavuni na Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi.

Mwaka jana Yanga walitwaa Kombe la Shirikisho Tanzania (FA) kwa kuichapa Azam FC mabao 3-1, mabao hayo yakifungwa na Amissi Tambwe aliyefunga mawili na jingine Deus Kaseke, lile la Azam lilifungwa na Didier Kavumbagu.

Pia Niyonzima alitwaa Ngao ya Jamii mara tatu, ambapo mara yake ya kwanza ilikuwa msimu wa 2013/14 baada ya kumaliza nafasi ya pili na Azam kuibuka mabingwa, hivyo kwenye mechi ya mchezo huo dhidi ya Azam, Yanga walishinda bao 1-0 lililofungwa na Salum Telela, msimu uliofuata waliwafunga tena Azam mabao 3-0, ambayo yalifungwa na Geilson Santo ‘Jaja’ mawili na Simon Msuva kufunga moja na kunyakua tena Ngao ya Jamii.

Niyonzima aliisaidia Yanga kunyakua Ngao ya Jamii kwa mara ya tatu msimu wa 2015/16, wakicheza tena mechi ya ufunguzi dhidi ya Azam na kushinda kwa penalti 8-7, baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya bila kufungana katika dakika zote 90.

Msimu wa 2016/17, Niyonzima na kikosi chake cha Yanga, kilishindwa kutetea taji hilo baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-1 dhidi ya Azam, baada ya mchezo wa kawaida kumalizika kwa sare ya 2-2.

Huu ni msimu wake wa kwanza wa Niyonzima tangu atue Simba na tayari ameuanza kwa kunyakua taji la Ngao ya Jamii, baada ya Wekundu hao wa Msimbazi kuwachapa Yanga kwa mikwaju 5-4 ya penalti, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0.

Je, nyota huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda, Niyonzima mwenye umri wa miaka 27, ataendeleza kismati chake cha mataji akiwa Simba katika miaka yake miwili au zaidi kama ataongezewa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -