Tuesday, January 19, 2021

NIYONZIMA, HAKIKA UNAZILAINISHA KURASA NGUMU KUSOMEKA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HALID MTUMBUKA

MICHAEL Jackson ni mmoja kati ya wanamuziki walioifanya dunia ya wapenda muziki kuupenda maradufu muziki wake. Michael Jackson aliifanya dunia kuwa rahisi mno kwa wapenda muziki na hata wale ambao hawakuzaliwa na vinasaba vya kuupenda muziki kwenye miili yao, walipenda vitu vichache kutoka kwake.

Ni yeye aliyependwa kutokana na aina yake ya uchezaji jukwaani na ni yeye aliyeifanya mioyo laini ya wasichana warembo kuongeza mapenzi yao maradufu kwenye tasnia hiyo. Dunia ilishuhudia mtu aliyeufanya muziki kupenya mioyoni mwa wapenda muziki.

Mwigizaji Steven Kanumba aliifanya tasnia ya uigizaji Tanzania kupendwa na hata wasiopenda filamu za Kitanzania. Huyu ni mwanamume aliyeaminika kwamba kaburi lake lilifunika vitu viwili. Cha kwanza ni mwili wake na cha pili ni ubunifu mzima wa tasnia hiyo.

Kuna watu wamezaliwa kwa kazi moja tu duniani, kuifanya kazi yao kupendwa na hata wasiopenda kazi zao. Yupo binadamu mmoja aliyenifanya niyakumbuke majina mawili niliyoyataja hapo juu baada ya kuishuhudia kazi nzuri aliyokuwa akiifanya uwanjani, huyu ni Haruna Niyonzima.

Haruna Niyonzima anaufanya mpira kupendwa na hata wasioupenda mpira. Ni mmoja kati ya binadamu wachache wanaozifanya ipasavyo kazi zao na kuwavutia wengine wazipende kazi zao. Ni nani asiyetamani kumuona Niyonzima uwanjani? Ni mrembo gani asiyependa kumuona Niyonzima? Hata kama asipoupenda mpira, atampenda tu Haruna Niyonzima.

Sababu hii ya kutimiza majukumu yake ipasavyo uwanjani na kuwa mwenye mwendelezo wa kile kilicho bora kutoka kwenye miguu yake, ndicho kinachowafanya hata makocha na viongozi wa timu nyingine kutamani kufanya naye kazi.

Ndiyo, kwani wakati wa ufunguzi wa dirisha dogo la usajili, timu ambayo ni kifurushi cha kushtua msimu huu, Mbao FC ilinukuliwa ikisema inahitaji wachezaji wenye ubora kama wa Niyonzima.

Tunatarajia kuimarisha kikosi chetu kwa kupata wachezaji wenye ubora kama Niyonzima na Mavugo kwa ajili ya mzunguko wa pili” hii ni kauli ya kishujaa inayotambua uwezo na mchango wa binaadamu huyu.

Ulishuhudia alichokifanya alipotolewa Amissi Tambwe kwenye eneo la ushambuliaji? Aliingia Said Juma Makapu ambaye ni kiungo asilia wa ulinzi. Ungeweza kumshangaa Lwandamina siku ile na usingeweza kumwelewa milele.

Lakini alijua ubora wa mchezaji wake hasa kwenye kupiga pasi za mwisho zinazofungua mianya kwa timu kupata ushindi.

Kilichofuata ni Haruna Niyonzima kupanda juu kucheza kama mshambuliaji namba mbili mwenye majukumu ya kumlisha Ngoma, Msuva na Kaseke waliokuwa wakitokea pembeni na kuitanua idara ya ulinzi ya JKT Ruvu.

Bakari Shime kocha wa JKT Ruvu, aliingia kwa kukaba mno hasa kwenye idara yake ya ulinzi iliyokuwa na nidhamu mno ya ukabaji kwenye kipindi cha kwanza.

Tulishuhudia sana Msuva na Kaseke wakitumika katika kupandisha mashambulizi. Nidhamu kubwa ya Michael Aidan, Edward Charles na wenzake ilianza kushuka mara tu baada ya Niyonzima kusogea juu na sekunde chache tu Msuva akapata bao.

Niyonzima ndiye aliyekuwa ‘Playmaker’ wa Yanga siku ile. Licha ya kutocheza vizuri kipindi cha kwanza, Yanga walistahili ushindi kwenye mchezo wa leo. Ndiyo maana baada ya mchezo kocha Lwandamina aliandika kwenye akaunti yake juu ya vijana wa Yanga kushinda.

Lwandamina alisema: “Vijana walistahili ushindi,” ni kweli. JKT Ruvu hawakuonekana kuwa na mipango asilia ya kutafuta ushindi ikiwamo kushindwa kuutumia uwazi katikati ya Vincent Bossou na Kelvin Yondani, ambao mara kwa mara walikuwa wakiacha uwazi katikati yao.

Nilijisemea moyoni mwangu, ahsante sana Haruna Niyonzima kwa kukifungua kitabu cha ‘Mchawi Mweusi’, Bakari Shime. Hata kama huupendi mpira na huipendi Yanga, lazima utazipenda tu pasi za Niyonzima, mijongeo yake na namna anavyofungua kurasa ngumu kusomeka na kuzilainisha. Niyonzima utaishi maisha marefu ya mpira, sijawahi kuwa mtabiri ila acha tuamini kwamba ukifuata miiko ya maisha, utaishi maisha marefu.

Thamani yake uwanjani inakwenda sawa na thamani yake sokoni. Huyu ni nyota anayepanda kila kukicha uwanjani na sokoni, anajua jinsi ya kuifanya kazi yake na thamani ya miguu yake.

Tangu alipotua nchini mwaka 2011, Haruna Niyonzima amekuwa na mafanikio yaliyomwezesha kuongeza dau lake kila anapoongeza mkataba.

Huu ni mwaka wake wa sita nchini baada ya kuongeza mkataba mara mbili jambo linalomfanya kuwa mchezaji wa kigeni aliyedumu zaidi katika klabu ya Yanga.

Mengi yamesemwa kuhusu Niyonzima lakini ukweli unabaki kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji wa kigeni waliovuna mamilioni katika soka la Tanzania.

Kwa hesabu za haraka haraka tena bila kujumlisha posho na marupurupu mengine, Niyonzima amevuna zaidi ya shilingi milioni 680 katika malipo ya usajili na mishahara yake.

Dau la dola 30,000 na mshahara wa dola 1500 ulimng’oa APR mwaka 2011 kwa mkataba wa miaka miwili.

Mwaka 2013, dau lake lilipanda zaidi baada ya kufanikiwa kuongeza mkataba wa miaka miwili tena kwa kitita cha dola 75,000 na mshahara wa dola 2500 kwa mwezi.

Mwaka 2015, wakati wengi wakiamini uwezo wake umepungua, Niyonzima alionesha umakini kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba kwa kutamka wazi kuwa yuko tayari kutua Simba au Azam.

Kwa namna fulani, jambo hilo lilimsaidia kupewa mkataba wenye maslahi zaidi. kwa mshahara unaotajwa kuwa dola 30,000 na dau la dola 60,000 alianguka saini ya kuendelea kuvaa jezi za rangi ya kijani na njano kwa miaka miwili zaidi.

Licha ya mapungufu yake mengine ndani na nje ya uwanja, Niyonzima amekuwa akipanda dau kwa sababu ya kujiamini na kutambua ‘wakati wa kupambania maslahi yake kwa kuonesha kiwango cha kuwafunga mdomo wakosoaji’.

Mwaka 2013, akijua kabisa mkataba wake unaelekea ukingoni alionesha kiwango cha hali ya juu ikiwamo kufunga bao tamu na la ushindi dhidi ya Azam.

Msimu huu tena, hasa katika mechi tano za mwisho, Niyonzima anaonesha ni jinsi gani anastahili kuendelea kuwapo Yanga.

Kwa kiwango chake cha sasa kinachopelekea baadhi ya mashabiki wa Yanga kutamba,” mwenye mpira wake karudi’ na kumsahau Thaban Kamusoko nani ana ujasiri wa kusimama na kudai jamaa hafai kuendelea kuichezea Yanga? Nani mwenye moyo wa ujasiri anayeweza kuja mbele yetu kutuambia hafai?

Nakumbuka kipindi kile alipotaka kuachwa kwa sababu za utovu wa nidhamu. Najaribu kuvuta picha kwamba wale waliohitaji kumtoa kafara bado wanaweza kudiriki kufanya hivyo? Huyu ndiye Niyonzima, hakika anazilainisha zile kurasa zote zilizongumu kusomeka na kuufanya mchezo wa soka kuwa rahisi mno machoni mwetu.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -