Wednesday, October 28, 2020

NIYONZIMA: SI RAHISI KUTETEA TAJI BARA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO mshambuliaji na ndiye nahodha wa sasa wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema wanatakiwa kuvuja jasho kama wanahitaji kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Niyonzima alisema kutokana na Simba kuendelea kushinda michezo yao, kazi inatakiwa kufanyika kwani si rahisi kutetea taji lao msimu huu.

Kiungo huyo alisema licha ya wao kuendelea kushinda kwa baadhi ya michezo, lakini wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanawafikia wapinzani wao Simba.

Alisema ili waweze kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea taji lao, wanatakiwa kuendelea kushinda lakini wakiomba Simba kupoteza angalau michezo yao miwili.

“Tayari tupo nyuma kwa pointi nne dhidi ya Simba, ili tuweze kutetea taji letu lazima tuwafikie na kuwapita kwa alama na jambo hili wanatakiwa wenzetu wapoteze na sisi kushinda katika michezo yote iliyosalia.

Kihesabu unaweza kuona rahisi lakini si kazi rahisi kwa kuwa wapinzani wetu nao wanajipanga kuhakikisha wanaendelea kusonga mbele,” alisema.

Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 44, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 40 baada ya kila timu kucheza michezo 18.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -