Monday, October 26, 2020

No Modrick, No Party Bernabeu

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

REAL Madrid haiko sawa. Ni rahisi kusema hivi kwa sasa na ukaeleweka.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006, Madrid wamepata sare nne kwenye michezo minne mfululizo. Ni ajabu lakini ni kweli imetokea.

Unajua tatizo lilipo? Linaweza kuwa swali gumu kulipatia majibu kama utajiuliza haraka haraka na kujijibu haraka haraka pia.

Kuna tatizo na njia rahisi ya kulifahamu ni kulirudia tena kulitazama pambano lao dhidi ya Eibar. Bila Luka Modric, Madrid inacheza bila mpango wowote.

Mwanzoni mwa msimu, wakiwa na Modrick, vijana wa Zinedine Zidane walishinda michezo mitano mfululizo, lakini ghafla mambo yakageuka na kutoka sare nne mfululizo, dhidi ya Villarreal, Las Palmas, Borussia Dortmund na Eibar.

Villarreal walimaliza kwenye nafasi ya nne msimu uliopita kwenye La Liga, bado halikuwa tishio kubwa kwa Madrid.

Las Palmas wamepanda daraja msimu huu, zilikuwa pointi tatu za lazima kwa Zidane, angalau hili la Dortmund linaweza kuelezeka na likaeleweka.

Kucheza na kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Dortmund msimu huu tena wakiwa kwenye uwanja wao wa Signal Iduna Park, ni jambo gumu linalohitaji utayari mkubwa ndani yake.

Hivyo Zidane anaweza kuwa na sababu ya kuongea, lakini kukosa pointi tatu dhidi ya Eibar, tena pale Santiago Bernabeu, hapa Zidane hana cha kujitetea zaidi ya kujieleza.

Ndiyo, Madrid haiko sawa tangu walivyompoteza Casemiro katikati ya uwanja, hawajashinda mchezo wowote tangu alipopata jeraha dhidi ya Espanyol. Ni kweli Casemiro alikuwa nguzo ya ulinzi kwa Madrid, lakini kukosekana kwake hakuwezi kuwa sababu ya wao kushindwa kuifunga Eibar.

Hata bila ya James Rodriguez na Luka Modric aliye nje akiuguza jeraha la goti, bado Zidane alitakiwa awe na mbinu za kupata ushindi dhidi ya Eibar, ulikuwa mchezo rahisi sana kwao.

Walivurugana kwenye safu yao ya ulinzi wakati Fran Rico akiipatia Eibar bao la kuongoza, lakini baada ya kusawazisha kupitia kwa Gareth Bale, aliyefunga kwa kichwa krosi ya Cristiano Ronaldo, mabingwa hawa wa Ulaya walitakiwa kutafuta matokeo zaidi, kwanini walipooza?

Hapa utaelewa kwanini bila Modric, Madrid inapoteza mwelekeo kabisa wa namna ya kucheza na kupata muunganiko mzuri kutoka kati ya uwanja hadi mbele.

Sifa ya Madrid ni kucheza soka la kushambulia muda wote, unapokuwa na Ronaldo na Bale kwenye safu ya ushambuliaji, ni lazima uione timu ikicheza kwa kulazimisha muda wote.

Ronaldo alifanya kazi nzuri kumtengea nafasi Bale na kupata bao, lakini Mreno huyu alipoteza nafasi nyingi za wazi na hii ilijidhihirisha kuwa nyota huyu hajarudi kwenye kiwango chake tangu zilipomalizika fainali za Euro 2016 kule Ufaransa.

Achana na Ronaldo, Alvaro Morata aliichangamsha sana safu ya ushambuliaji alipoingia kuchukua nafasi ya Karim Benzema, lakini straika huyu wa Kihispania alipata shida sana kuipenya ngome ya Eibar, kwanini? Hakukuwa na nafasi nzuri zilizokuwa zikija mbele yake.

Masikini Isco, wakati huu anapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini bado hajaweza namna ya kuiendesha timu katikati ya uwanja, hapendwi pia na mashabiki wake wa Santiago Bernabeu.

Alipoteza mipira mara nyingi, alikosa nafasi za wazi, hakuweza kuifanya safu ya ushambuliaji ipate nafasi za wazi, halikuwa jambo la ajabu kuona akifanyiwa mabadiliko dakika 18 kabla ya pambano kumalizika.

Dhidi ya Eibar, Madrid walikuwa na Ronaldo, Bale, Benzema, Morata, Isco na Marco Asensio kwa pamoja uwanjani, hapa unategemea kuona wakiwa na uchu wa mabao na kuiweka taabani safu ya ulinzi ya Eibar, lakini hali haikuwa hivyo.

Bila Casemiro na Modric, Madrid inaonekana kuanza kuwa mzigo mzito kwa Zinedine Zidane – na kama gwiji huyu wa soka duniani asipotuliza kichwa na kulitafutia ufumbuzi tatizo hili, bila shaka atakuwa anajiweka kwenye mazingira magumu sana mbele ya Rais Florentino Perez. Nani asiyeyajua maamuzi ya kiwendawazimu ya Rais huyu?

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -