Friday, November 27, 2020

NYIE MCHEKENI TU, HARMORAPA ATAENDELEA KUTUSUA NA KIKI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

KIKI si kitu kigeni kabisa kwa wasanii ulimwenguni ambapo maana halisi ya neno hili ni kutafuta jambo la kushtukiza na kuwafanya mashabiki wamzungumzie msanii husika kwa muda mrefu zaidi.

Kiki hutumika kutafuta zaidi kuongelewa zaidi kwenye televisheni, redio na kwenye mitandao ya kijamii ambapo wasanii wamekuwa wakitafuta njia hii ili kusaidia kazi zao kusikilizwa zaidi.

Kwa kawaida kiki ni nzuri na humsaidia msanii kumpandisha kiwango ambapo kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wasanii kutengezeza stori ambayo itavuta hisia za wengi katika mitandao ya kijamii ili tu azungumziwe sana.

Wapo mastaa mbalimbali Bongo ambao wametingisha kwa kiki na kufanya wazungumziwe sana na matokeo yake kupata faida ya kufanya promo kwa kazi wanazozifanya.

Wasanii hao baadhi ni Ruby na Aslay walikuwa wakiandaa wimbo wa Ni Wewe, waliwahi kutangaza kuwa na mahusiano ya kimapenzi kumbe walikuwa wakitafuta kiki tu na wala si vinginevyo.

Lakini kulikuwa na mcheza filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’, ambaye aliwahi kufanikiwa kuwakamata watu kwa kutengeneza kiki yenye akili kuwa mabadiliko yake ya rangi yalitokana na kunywa maji mengi jambo lililomfanya kuzungumziwa kila sehemu.

Wakati mambo hayo yakiendelea hivi karibuni ameibuka msanii aliyejiita Athumani Omary ‘Harmorapa’, akiwa anafanana sana na mwanamuziki, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ aliye chini ya lebo ya WCB.

Hakuna aliyekuwa anamjua Harmorapa hapo awali, lakini kiki zake za kila kukicha zimewafanya kila mtu kumtolea macho kumwangalia msanii huyo ambaye tayari ametoa wimbo wake unaojulikana kwa jina la Usigawe Pasi.

Alianza kama utani vile na kiki ya kufananishwa na Harmonize ambapo hapo alipachikwa jina la ‘Kiboko ya Mabishoo’, jina ambalo linaendelea kumbeba kila kukicha.

Harmorapa akaja na staili nyingine ya kumpigia goti msanii, Ali Kiba, alipoibuka kwenye mapokezi yake pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) alipokuwa anawasili kutoka Afrika Kusini alipotoka kuchukua tuzo ya MTV.

Alipofanya tukio hilo jina lake lilizidi kujaa masikioni mwa mashabiki mbalimbali wa burudani ambapo wengi walimtaja kama msanii aliyeingilia bifu la Ali Kiba na Nassib Abdul ‘Diamond’.

Hamorapa aliendelea kutafuta kiki baada ya kuweka video kwenye kurasa zake mbalimbali akionyesha kuwa na fedha nyingi ambazo baadaye zilitajwa kuwa ni za meneja wake.

Tukio ambalo wengi hawakulitarajia ni msanii huyo kuonekana kwenye ofisi za Clouds Fm eti akitoa pole baada ya watangazaji wake kushikiwa bastola kwenye tukio lililotokea mwezi huu.

Achana na pole, mbio alizotoka wakati wa tukio la kuonyeshwa bastola kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, limemfanya jina lake kuendelea kuwamo kwa mashabiki wake mbalimbali.

Staili nyingine aliyoingia nayo kama gia ni ‘kumtusi’ Moses Iyobo, mpenzi wa Aunt Ezekiel kuwa mkata viuno hawezi kubishana naye jambo lililomfanya kupata mashabiki wengi zaidi kusikiliza wimbo wake wa Kiboko ya Mabishoo aliomshirikisha mkongwe, Juma Nature.

Ni dhahiri Harmorapa anatumia kiki zake vema ambazo zinamsaidia kujitangaza na kuendelea kujitengenezea jina kwenye soko la muziki ambalo kwa sasa ndilo lenye mashabiki wengi zaidi.

Wengi walidhani kama utani pale alipoanza kiki ili kujitangaza lakini kwa sasa amekuwa ndiyo stori ya mjini na kila mmoja kutamani kumsikia kila kukicha hivyo kuzidi kuzinadi kazi zake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -