Friday, December 4, 2020

Nyota Simba kulindwa kwa kifaa maalum

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MOHAMED KASSARA

KATIKA kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika michuano ya Afrika, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘MO’, ameagiza kifaa cha kufuatilia mienendo ya wachezaji kinachofahamika kama GPS.

Teknolojia hiyo ya GPS, itamrahisishia kocha wa timu hiyo  kufuatilia mienendo ya wachezaji kuanzia mazoezini na hata nje ya uwanja, kufahamu wale wasiojituma, walevi na wale wanaokesha kwenye starehe na kuchelewa kulala.

Mbali ya GPS, MO aliahidi kuwekeza katika kituo cha lishe (Nutrition Center), kujenga viwanja viwili vya mazoezi, hosteli, kuwekeza kwenye kituo cha kurudishia utimamu (Recovery) na taaluma ya kuchua misuli (Massage) pamoja na watalaamu wa saikolojia.

Akizungumza jana Dar es Salaam wakati wa mahojiano na Wasafi Redio, MO, alisema ili kufanya vizuri kimataifa, ni lazima kuzingatia vitu kama  hivyo  ambavyo wakati mwingine vimekuwa vikiikwamisha timu hiyo dhidi ya timu nyingine Afrika.

Alisema klabu kubwa Afrika zimewekeza katika maeneo hayo na wakichagizwa na usajili mzuri wanaoufanya ndiyo maana wamekuwa wakifanya vema na kuwa tishio katika michuano hiyo.

“Tumegundua wenzetu wanatumia teknologia sana na mara hii nimeagiza  mfumo wa GPS kuweza kufuatilia wachezaji, kuna wachezaji wengine wavuvi, kwahiyo kocha anaweza kuchunguza huyu mchezaji anajituma, kwa sababu inahusisha mapigo ya moyo, mapigo ya moyo wake yakiwa juu, atajua hapa nafanya kazi.

“Pia, tunaweza kujua huyu kijana ameingia kulala saa ngapi, ameamka saa ngapi na kama mfano amepiga pombe zake, mapigo yake ya moyo yanapanda, hivyo, tutajua hapa kuna tatizo. Pia, tutawekeza katika eneo la saikolojia; mchezaji anaweza kuja hajacheza mechi tatu.., nne, anaanza kukata tama. Lazima kuwe na mtu wa kuwapa moyo na kurudishia hali ya upambanaji,” alisema MO.

MO aliongeza kuwa atawekeza kwenye timu za vijana kuanzia chini ya miaka 18 hadi 12 ili kuwaanda wachezaji chipukizi wenye utamaduni wa klabu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -