Wednesday, November 25, 2020

AMINI MKOSA: NYOTA WA KIKAPU BONGO ANAYEGOMBANIWA AFRIKA KUSINI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SHARIFA MMASI

MIONGONI mwa nyota wa Tanzania wanaocheza mpira wa kikapu anayetabiriwa makubwa siku za usoni ni kiungo, Amini Mkosa (21), anayekipiga katika klabu ya Savio, inayomilikiwa na kituo cha Don Bosco, kilichopo maeneo ya Upanga, jijini Dar es Salaam.

Nyota ya mchezaji huyo anayevaa jezi namba saba, ilianza kung’ara  tangu akikipiga katika timu ya Don Rua, kabla ya kupandishwa kucheza timu ya Don Bosco Young Stars.

Wakati akiwa Don Bosco Young Stars, alifanikiwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu kipindi chote alichowahi kushuka dimbani, kilichowashawishi viongozi wake kumpa namba kwenye timu kubwa ya Savio, klabu zote hizo zinamilikiwa na kituo cha Don Bosco.

Katika familia ya mpira wa kikapu nchini, jina la Mkosa linaendelea kutajwa na wengi, wakidai ni miongoni mwa viungo wanaofuata nyayo za Hasheem Thabeet, anayecheza Ligi ya Taifa ya Marekani ya NBA.

Kuendelea kutajwa kwa mchezaji huyo, kunasababishwa na kiwango anachokionyesha kupitia Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inayoendelea kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini.

Katika ligi hiyo iliyopo kwenye mzunguko wa kwanza, klabu ya Savio ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo, ikiwa kileleni mwa msimamo wa RBA kwa jumla ya pointi 16.

Hadi sasa Savio hawajapoteza mchezo hata mmoja katika ligi hiyo tangu washuke dimbani, huku baadhi ya mashabiki wakionekana kumtolea macho Mkosa kutokana na kuisaidia klabu yake kuibuka kidedea katika kila mchezo.

Mwandishi wa makala haya kupitia gazeti la BINGWA, amefanya mahojiano na kiungo huyo kujua mambo mbalimbali yanayomhusu, ikiwamo ya kimichezo na maisha kwa ujumla.

BINGWA:  Habari yako?

Mkosa: Salama namshukuru Mungu sijui wewe.

BINGWA: Binafsi sijambo, unazungumziaje maisha yako kimichezo ukiwa ndani ya klabu ya Savio?

Mkosa: Maisha yangu kimichezo kwa namna moja au nyingine, naweza kusema ni mazuri na mpira wa kikapu kwa ujumla ndio umenifikisha hapa nilipo.

BINGWA: Unataka kuniambia kwa umri huo ulionao unaishi kupitia mpira wa kikapu?

Mkosa: Naam! Wala hujakosea, ndiyo maana nikathubutu kutamka kwamba, bila mpira wa kikapu nisingekuwa hapa nilipo hivi sasa.

BINGWA: Katika safari yako ya kimichezo, kitu gani hutakuja kukisahau?

Mkosa: Namuomba Mungu kila siku, isije ikatokea siku wala saa nikausahau uongozi wa Don Bosco, ambao umenitoa mbali sana, kama ni mtoto mdogo basi nathubutu kusema nilikuwa nakaa hadi sasa nakimbia mbio ndefu.

BINGWA: Zipi fadhila zako kwa Don Bosco?

Mkosa: Moja ya fadhila ambazo naendelea kutoa kwa Don Bosco, ni kufanya yale ninayoelekezwa na kocha kipindi chote cha mazoezi, kupitia mashindano mbalimbali, yakiwamo haya ya RBA, ambayo hadi sasa Savio tunafanya vema.

BINGWA: Kuna tetesi zinadai mlipokwenda Afrika Kusini kucheza mechi za kirafiki, baadhi ya klabu za vyuo vikuu zilivutiwa na kiwango chako, je, kuna ukweli wowote juu ya hilo?

Mkosa: Bila shaka wala kificho, kuna klabu za vyuo (jina lipo kapuni) zilivutiwa na kiwango changu na hivi ninavyokwambia uongozi wangu upo kwenye mazungumzo mazito kufikia mwafaka.

BINGWA: Unafikiri fursa ya klabu za nje kukuhitaji imekuja wakati mwafaka kwako?

Mkosa: Haswaa, fursa imekuja wakati mwafaka.

BINGWA: Unaweza kuwaambia mashabiki wako, kiasi cha fedha unachohitaji kulipwa ili ukatumikie klabu za nje?

Mkosa: Kwa sasa sipo tayari, kama nilivyosema uongozi wangu ndio kila kitu, mambo yatakapokuwa tayari nitafunguka na mashabiki wangu wataelewa kinachoendelea.

BINGWA: Changamoto gani umekumbana nazo kipindi hiki ambacho mnaongoza kwenye ligi ya RBA?

Mkosa: Changamoto ni zakawaida tu, ambazo wahusika, Chama cha Mkoa wa Dar es Salaam (BD) hawana budi kuzirekebisha mapema kabla ya kuingia mzunguko wa pili, unaotabiriwa kuwa na upinzani mkali kuliko hivi sasa.

BINGWA: Ipi siri ya mafanikio yenu inayoendelea kuwapa ushindi katika kila mchezo?

Mkosa: Siri kubwa inayoendelea kutuweka kileleni ni kujituma, ushirikiano ndani na nje ya uwanja, pia klabu yetu imemsajili kocha mwenye kiwango cha kimataifa ambaye ni Evaristi Mapunda, aliyewahi kuifundisha klabu ya Pazi, inayoshiriki RBA.

BINGWA: Upi ushauri wako kwa vijana mitaani.

Mkosa: Nawashauri vijana wenzangu wajitume katika harakati zao za kutafuta maisha, wakishindwa tunawakaribisha kwenye michezo, kwani hata huku kunalipa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -