Friday, October 30, 2020

NYOTA WATANO WAFUNGIWA VIOO YANGA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

BAADA ya Yanga kupata sare ya kufungana bao 1-1 na African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa matokeo hayo yamewaweka matatani wachezaji watano nyota wa timu hiyo.

Matokeo ya mchezo huo uliochezwa Ijumaa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, yalihusishwa na mgomo baridi wa siku mbili mfululizo wa kugomea mazoezi uliowekwa na wachezaji wakishinikiza kulipwa mshahara.

Kutokana na matokeo hayo, baadhi ya wachezaji wameanza kuisoma namba kwa kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina, kuwaondoa katika programu yake ya mazoezi ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.

Wachezaji wanaotajwa kuondolewa katika programu ya Lwandamina ni pamoja na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Malimi Busungu, Oscar Joshua, Pato Ngonyani na Antony Matheo.

Pamoja na wachezaji hao kuendelea kuruhusiwa kufanya mazoezi na wenzao, lakini inapofikia timu kwenda kambini kwa ajili ya kuwapa mbinu zaidi hawatakiwi kutia mguu, suala hilo limehusishwa na madai kadhaa ikiwemo kushindwa kumshawishi kocha wao na kushuka kwa viwango vyao.

Nyota hao hawakujumuishwa katika kambi ya pamoja ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Ndanda uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru na kushinda mabao 4-0, kutokana na madai mbalimbali.

Katika maandalizi ya mchezo huo, wachezaji 18 ndio walioingia kambini ambao ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Emmanuel Martin, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Andrew Vincent, Ali Mustapha ‘Barthez’, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Simon Msuva, Said Juma, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Justin Zulu, Geofrey Mwashiuya, Obrey Chirwa  na Thaban Kamusoko.

Lakini Barthez, Mwashiuya, Chirwa na  Hassan Ramadhan ‘Kessy’, wenyewe wapo  chini ya uangalizi maalumu kutokana na viwango vyao kuonekana kushuka, hivyo wametakiwa kupandishwa viwango ili kuendelea kumshawishi kocha wao, vinginevyo wanaweza kupoteza namba kabisa katika kikosi chake.

Imeelezwa kwamba, kundi la akina Barthez limepewa nafasi ya kuonyesha uwezo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kesho kwenye Uwanja wa Amaan, kisiwani Unguja.

Mtoa habari wetu, alisema Lwandamina tayari amewaonyesha mlango wa kutokea nyota hao watano baada ya kushindwa kumshawishi katika mazoezi yake na kinachosubiriwa ni wamalize mikataba yao.

“Mwakani katika usajili wa dirisha kubwa kocha atakuwa na nafasi nzuri ya kusajili wachezaji wengi wazawa na tayari amewaona katika timu mbalimbali anachokifanya kwa sasa ni kumalizia kazi nzuri aliyoianza Hans van der Pluijm,” alisema mtoa habari wetu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -