Sunday, October 25, 2020

NYOTA YA JAA: MCHEKESHAJI MWENYE KIU YA KUMFUNIKA JOTI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MITANDAO ya kijamii imekuwa jukwaa jipya kwa wasanii kuonyesha vipaji vyao, kwani utandawazi umetoa nafasi kwa mashabiki kupata bidhaa za sanaa kwa urahisi zaidi kupitia vifaa vyao vyenye uwezo wa intaneti.

asani wa vichekesho ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mitandao ya kijamii. Utakuwa shahidi wa hili kama unafuatilia tasnia ya ucheshi nchini, kwani wachekeshaji wengi nguvu zao wamezielekeza huko mtandaoni.

Bakari Ngwere maarufu kama Nyota ya Jaa, ni mchekeshaji chipukizi anayetumia mitandao ya kijamii ya Istagram, Facebook na YouTube kufanya sanaa yake ya ucheshi.

Hivi karibuni jijini Dar es Salaam, BINGWA limefanya mahojiano na mchekeshaji huyo ili kufahamu zaidi namna anavyofanya kazi, changamoto na mafanikio anayoyapata kupitia ucheshi katika mitandao ya kijamii, karibu.

BINGWA: Mara nyingi familia hasa wazazi wanakuwa na wasiwasi kumruhusu mtoto wao kuingia kwenye sanaa, kwa upande wako hali ikoje?

Nyota: Mama na baba hawajawahi kunikataza ila walikuwa na wasiwasi tu kwa kuwa walidhani sanaa ni kitu ambacho kinaweza kunipotezea muda.

BINGWA: Kuna wachekeshaji wa mitandaoni kama vile Dullvan, Jay Mond, Uswege na wengine, je, wanakupa changamoto yoyote?

Nyota: Hawanipi changamoto ila tu wamenizidi nafasi, wao wanafahamika sana mimi ndiyo nakuja lakini kwenye uchekeshaji Dullvan na Jaymond kwangu ni chamtoto.

BINGWA: Kuna binti anaitwa Catherine ambaye huwa unachekesha naye, unadhani kwanini mashabiki wenu wanadhani mpo kwenye mapenzi?

 

Nyota: Ni kwa sababu ya ukaribu wetu, kila ninapokuwa mimi na yeye yupo, picha nyingi anazopiga basi na mimi nakuwepo hilo ndilo limefanya wengi wadhani kuwa ni wapenzi, Catherine namuheshimu kama dada yangu, tupo kikazi zaidi.

BINGWA: Mpaka sasa uchekeshaji kwenye mtandao umekupa faida gani?

Nyota: Namshukuru Mungu napata simu nyingi za kazi kutokana na umaarufu wangu, bado sijapata mafanikio makubwa kifedha ila kwa haya machache nashukuru.

BINGWA: Una mipango ya kufanya kazi na wachekeshaji gani na kwanini?

Nyota: Kwanza ni mimi mwenyewe kuongeza juhudi kwenye kazi zangu ili siku nikitaka kuwashirikisha wachekeshaji wengine thamani yangu iwe juu, natamani sana kufanya kazi na Joti, Mkali Wenu, Tin White, Ebitoke na Kinye Mkali, ni watu ambao kazi zao nazikubali.

BINGWA: Baada ya Mzee Majuto kufariki dunia wiki iliyopita, unadhani ni nani anaweza kuvaa viatu vyake?

Nyota: Mzee Majuto alikuwa namba moja ila ndiyo hivyo kazi ya Mungu haina makosa, hakuna mbadala wake ataendelea kuwa yeye japo kuwa Joti naye anafanya vizuri na mimi nina kiu na mafanikio yake kwenye uchekeshaji.

BINGWA: Unaweza vipi kufanya sanaa yako bila kuwa na meneja?

Nyota: Ni ngumu ila nakomaa kwa sababu meneja hawezi kuja tu bila kuona kazi yako, ila milango ipo wazi kwa yeyote anayeona tunaweza kufanya kazi.

BINGWA: Una neno lipi la kumalizia kwa mashabiki wa vichekesho?

Nyota: Kikubwa ni sapoti yao, wanaweza kutembelea chaneli yangu YouTube natumia jina la Nyota ya Jaa ili kuvunja mbavu zao.

BINGWA: Asante kwa muda wako.

Nyota: Shukrani sana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -