Saturday, November 28, 2020

OBREY CHIRWA APATIWA ‘KIZIZI’ CHA MABAO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

BAADA ya kushindwa kufunga bao katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia, mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, amepewa tiba itakayomwezesha kufanya vitu vyake wakati timu hizo zitakaporudiana jijini Lusaka, Zambia Jumamosi hii.

Tiba hiyo si nyingine bali ni kiungo mwenye uwezo wa hali ya juu wa kupiga pasi za mabao, Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

Niyonzima aliukosa mchezo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na sasa ameandaliwa rasmi kuhakikisha anamlisha vilivyo Chirwa jijini Lusaka na hivyo kuiwezesha timu yao kusonga mbele hatua ya makundi.

Yanga watakwea pipa leo kuwafuata wapinzani wao hao ambapo ili waweze kusonga mbele, watatakiwa kuibuka na ushindi wowote au kupata sare ya zaidi ya mabao 2-2.

Sambamba na hilo, Yanga wataendelea kumkosa mshambuliaji wao, Amissi Tambwe, katika mchezo huo wa Jumamosi kwani bado ni majeruhi.

Akizungumza na BINGWA nyumbani kwake Sinza Madukani jana, straika huyo alisema anasikitika kuukosa mtanange huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nkoloma uliopo Lusaka.

“Kwanza nasikitika kuukosa tena mchezo wa pili, nakabiliwa na majeraha makubwa ya goti ambayo yananilazimu kuendelea kukaa nje kwa zaidi ya wiki tatu mpaka nne. Kwa hiyo sitaweza kuambatana na timu,” alisema Tambwe.

Alisema goti lake limepatwa na tatizo la damu kuganda ndani na kuufanya mguu wake kuwa mzito wakati wa kukimbia pamoja na kuhisi maumivu makali wakati wa kuukunja mguu.

Aliongeza kuwa kutokana na majeraha hayo, leo hatasafiri na timu na kuwataka wachezaji wenzake kwenda kupambana kufa na kupona kuhakikisha wanarudi na ushindi.

“Kukosekana kwangu au mtu mwingine si mwisho wa wao kushindwa kupata ushindi. Nina imani tukiwa ugenini tunakuwa na bahati kuliko hapa nyumbani, naamini tutashinda,” alisisitiza straika huyo.

Kuelekea pambano hilo, mbali ya Tambwe, Yanga itamkosa mpachikaji mabao hatari, Donald Ngoma ambaye ni majeruhi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya timu hiyo, Paulo Malume, amesema kuelekea katika mchezo huo, timu ipo kamili ikiwa ni baada ya matajiri wao kumaliza matatizo ya kifedha yaliyokuwa yakiwakabili wachezaji.

“Tunaenda kufanya maajabu kule na kwa taarifa yako tayari ujumbe mzito umeshatangulia kwenda (Zambia) kuweka mambo sawa. Tunakwenda kushinda, amini hivyo,” alisema Malume.

Msafara wa Yanga utakuwa na wachezaji 20 na viongozi 10 na utasafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya Airways.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -