Monday, January 18, 2021

OKWI AANZA NYODO SIMBA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

WINFRIDA MTOI NA SALMA MPELI

KUNA msemo usemao ‘ukimsifia mgema, tembo hulitia maji’. Ndivyo ilivyotokea kwa nyota wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye baada ya kumwagiwa sifa kila kona kutokana na kiwango chake akiwa na timu hiyo na timu yake ya Taifa ya Uganda, hatimaye ameanza nyodo zake.

Akifahamu jinsi watu wa Simba wanavyomkubali, kumthamini na kumheshimu, mshambuliaji huyo jana amewaweka njiapanda kutokana na kushindwa kutokea mazoezini kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Baada ya mchezo wao dhidi ya Azam FC mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini, wachezaji wote wa Simba walipewa mapumziko ya siku moja na jana walianza mazoezi rasmi kujiandaa na mechi yao inayofuata ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC, itakayochezwa Uwanja wa Uhuru, Jumamosi hii.

Okwi aliyewapa raha mashabiki wa Simba kwenye mchezo wa kwanza wa ligi baada ya kutupia mabao manne peke yake katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, aliikosa mechi dhidi ya Azam FC iliyoishia kwa suluhu.

Katika mchezo huo, Okwi aliushuhudia akiwa jukwaani kutokana na kuchelewa kufika nchini akitokea Misri alikokwenda kuitumikia timu yake ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’, ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Kwenye kikosi hicho cha The Cranes, pia yupo beki wa kati wa Wekundu wa Msimbazi hao, Jjuuko Murushid ambaye naye anaunda ‘first eleven’.

Juu ya kukosa kwake mazoezi ya jana asubuhi, inadaiwa kuwa Okwi alitoa taarifa kwamba ameamka akiwa na maumivu ya kichwa hivyo kuomba kumpumzika.

Wakati Okwi akitoa taarifa kwa simu, mchezaji mwenzake, Haruna Niyonzima, yeye alifika mazoezini asubuhi kabla ya programu kuanza na kuomba ruhusa kwa daktari wa timu hiyo kuwa tumbo linamsumbua na kupewa dawa kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Akizungumza na BINGWA, Daktari wa timu hiyo, Yasin Gembe, alisema Okwi amewafahamisha kwa simu kuwa anaumwa kichwa na Niyonzima anasumbuliwa na tumbo, hivyo amewaacha wapumzike hadi watakapopata nafuu.

“Niyonzima alifika asubuhi mazoezini akaomba ruhusa kwa kuwa tumbo lilikuwa linamuuma, lakina kwa upande wa Okwi, yeye alitoa taarifa ameamka asubuhi, ameshindwa kutoka kwani kichwa kilikuwa kinamuuma,” alisema Gembe.

Akizungumzia juu ya wachezaji wengine ambao ni majeruhi, Gembe alisema Shomari Kapombe ameanza mazoezi mepesi na siku yoyote ataungana na wenzake katika mazoezi ya pamoja, huku kipa wao, Said Mohamed ‘Nduda’ akiwa bado anaendelea na matibabu ambapo muda wowote anaweza kuondoka nchini kwenda India kwa matibabu zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -