Tuesday, November 24, 2020

OKWI AIGEUKA SIMBA, ATUA JANGWANI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

WAKATI Simba ikihaha huku na kule kutaka kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi ndani ya klabu hiyo, straika huyo amewageuka mabosi hao wa Msimbazi na kutua Jangwani na leo atatua Uwanja wa Taifa wakati mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiivaa Azam.

Okwi, ambaye alivunja mkataba wake na kikosi cha SonderjyskE ya nchini Denmark, ni kipenzi cha mashabiki Simba alioonekana jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akiwa na mabosi mbalimbali wa Yanga.

Yanga inataka kumsajili Okwi ili kuboresha safu yao ya kiungo ili kujiimarisha zaidi msimu ujao na kuweza kutimiza malengo yao ya kuendelea kufanya vema kwenye michuano mbalimbali, hasa ya kimataifa.

Inajulikana kwa siku za karibuni, Kocha wa Yanga, George Lwandamina, amekuwa akipata tabu sana kwenye kikosi hicho kuteua ‘first eleven’, hasa baada ya nyota wengi tegemeo kuwa majeruhi, huku wengine wakitangaza kuondoka msimu ujao.

Lakini stori hii ya Okwi inaweza ikawa habari nzuri sana kwa mashabiki wa Yanga, kutokana na kutambua uwezo wake ambapo amewahi kuwafunga mara kadhaa akiwa na Simba, huku wale wa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi wakiwa na kilio kutokana na kumsubiri straika huyo kwa muda mrefu.

Okwi, ambaye kwa siku za karibuni ameendelea kung’ara nchini Uganda akiwa na kikosi cha SC Villa, huenda asionekane tena Simba na badala yake akivaa tena jezi hiyo ya Wanajangwani msimu ujao.

Poleni kwa wale waliopata taharuki, hasa wale mashabiki wa Simba, kwani leo ni Aprili Mosi, ambayo ni Siku ya Wajinga Duniani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -