Sunday, January 17, 2021

Okwi aikata maini Simba

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MWANDISHI WETU

EMMANUEL Okwi, anayekipiga Sonderiyske ya Denmark, amewakata maini mashabiki wa Simba waliokuwa na matarajio makubwa ya mshambuliaji huyo kurejea Msimbazi katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo, baada ya mpango huo kushindikana.

Hivi karibuni Simba walikuwa katika mchakato wa kumrejesha mshambuliaji huyo ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji, ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Taarifa za uhakika kutoka kwa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, zinasema kwamba Simba wamegonga mwamba katika mpango wao huo, baada ya uongozi wa Sonderiyski kuamua kutomwachia nyota huyo.

Mtoa habari wetu huyo alisema klabu hiyo ilikutana na wawakilishi wa Simba waliokwenda Denmark kwa ajili ya mazungumzo ambapo Senderiyski waliweka sharti la kwanza la kupewa Dola za Marekani 120,000 (zaidi ya Sh milioni 250) ili wamwachie Okwi.

“Dau hilo liliwafanya Simba kuwa na matumaini ya kumpata mchezaji huyo, lakini kwa upande wa Okwi, ameonyesha msimamo wake wa kutorejea nyuma na sasa anaangalia zaidi mbele, baada ya klabu yake hiyo kumng`ang`ania,” alisema.

Alipoulizwa juu ya Okwi, Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema mchezaji huyo hayuko katika mipango yao.

“Mambo ya usajili yapo chini ya Kamati ya Ufundi na Usajili, na hilo suala la Okwi halipo kabisa,” alisema.

Okwi ameendelea kuwa mchezaji anayependwa mno na mashabiki wa Simba kutokana na kukitumikia kikosi chao kwa ufanisi wa hali ya juu, zaidi akikumbukwa jinsi alivyowaongoza Wekundu wa Msimbazi hao kuwashushia kipigo ‘kitakatifu’ watani wao wa jadi, Yanga, walipowachapa mabao 5-0 mwaka 2012.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -