Tuesday, October 27, 2020

OKWI APEWA BAO LA KAGERE LA CAF

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMARI NA MWAMVITA MTANDA


 

BAO alilofunga Meddie Kagere wakati akiitumikia timu yake ya Taifa ya Rwanda dhidi ya Ivory Coast wiki iliyopita, limeonekana kumkuna mno Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na hivyo kuanza kazi ya kulihamishia kwa straika wake, Emmanuel Okwi.

Kagere alifunga bao hilo kwa kichwa akiwa pembeni ya lango la wapinzani wao jijini Kigali, akiunganisha krosi murua kutoka wingi ya kulia.

Bao hilo la Kagere lilikuwa la kufutia machozi kwa Amavubi waliopokea kipigo cha mabao 2-1, ukiwa ni mchezo wao wa pili wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu hizo zikiwa Kundi H.

Katika kuonyesha jinsi bao hilo lilivyomgusa Aussems, ameamua kulifungia kazi katika mazoezi yake ndani ya Simba kwa kuwanoa vijana wake jinsi ya kucheka na nyavu zaidi kwa kutumia staili iliyompa ushujaa Kagere mbele ya mashabiki wao jijini Kigali.

Mbelgiji huyo aliyetua Msimbazi msimu huu akichukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre, katika mazoezi yake ya jana jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterans, Dar es Salaam, alitumia muda mwingi kujenga mashambulizi ya kupitia krosi, huku zikielekezwa kwa Kagere na Okwi.

Aussems, alikuwa akiwaelekeza mastraika wake hao wawili wa kati jinsi ya kuzitumia vema krosi kutoka winga zote mbili, akiamini njia hiyo itawawezesha kuvuna mabao mengi zaidi kutokana na tatizo …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -