Friday, October 30, 2020

Okwi awawashia taa nyekundu Ambokile, Kitenge

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Lulu Ringo, Dar es salaam

Straika wa Simba Mganda Emanuel Okwi amewawashia taa nyekundu mastraika wenzie Eliud Ambokile na Alex Kitenge waliokua na twakwimu nzuri ya ufungaji katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Okwi jana katika mchezo dhidi ya Simba na Ruvu shooting ametimiza jumla ya magoli 7 sawa na Ambokile kutoka timu ya Mbeya City huku akipachika magoli matatu ‘Hat- trick’ sawa na mchezaji wa Stand United, Alex Kitenge.

Katika michezo miwili mfululizo Okwi amefunga jumla ya magoli matano ikiwa ni magoli mawili dhidi ya Alliance Fc na magoli matatu dhidi ya Ruvu shooting, rekodi hii inakua ya kipekee katika Ligi Kuu kwani kufika rekodi hiyo wachezaji wenzake hao walitumia mechi zaidi ya mbili kuwa na idadi hiyo ya magoli waliyokuwa nayo.

Okwi katika msimu uliopita ndiye aliyetoka kinara wa mfungaji bora wa ligi safari yake ya ufungaji ikianzia Uwanja wa Taifa akiifunga Ruvu shooting magoli manne ambayo yalichangia timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa magoli mengi  ya7-0 ambao rekodi inasimama hadi leo hii.

Hat Trick ya kwanza kwa msimu uliopita ilipachikwa Uwanja wa taifa sawasawa na msimu huu, Alex Kitenge aliifunga Yanga magoli matatu ambapo wanajngwani hadi dakika 90 zinakamilika  matokeo yalikuwa 4-3, hata hivyo hat trick za kwanza kwa Okwi katika msimu uliopita na huu zimepatikana dhidi ya Ruvu shooting mechi zote zikichezeka uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -