Saturday, October 31, 2020

Okwi, Kagere washikwa uchawi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI


MCHAMBUZI maarufu wa soka nchini, Alex Kashasha ‘Mwalimu Kashasha’, ametaja sababu ya Simba kushindwa kupata mabao katika mchezo wake na Yanga kuwa ni ubinafsi wa washambuliaji wake kila mmoja akitaka kufunga.

Simba na Yanga zilikutana juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam na kutoka suluhu.

Akizungumza na BINGWA jana jijini,  Kashasha alisema alivyotazama safu ya ushambuliaji ya Simba, licha ya kushambulia lakini ushirikiano wa  Emmanuel Okwi na Meddie Kagere haukuwa mzuri na hawakubadilika kutokana  na hali ya wapinzani wao.

Alisema sababu kubwa ya mastraika hao kushindwa kupeana ushirikiano ni kutokana na ukubwa wa mchezo ambao mchezaji akifunga anajitengenezea rekodi.

“Simba ni wazuri na wameweza kumiliki mpira kwa muda wote na kufanya mashambulizi, lakini nilichokiona Okwi na Kagere walikosa ushirikiano au unaweza kusema walikuwa na ubinafsi kila mmoja akitaka kufunga hata katika eneo ambalo haliwezekani,” alisema Kashasha.

Kwa upande wa Yanga, alisema walitumia mbinu mbadala ya kucheza kwa kujihami huku wakiimarisha ulinzi wakifahamu kikosi chao ni dhaifu na wamekutana na timu imara.

“Timu zote zilionekana kucheza vile kulingana na zilivyojipanga, tatizo lililoonekana ni kwa mchezaji mmoja mmoja lakini kimchezo mabenchi yote ya ufundi yalionekana kujiandaa,” alisema.

Alifafanua kuwa kutokana na hilo, kila timu inatakiwa kuboresha baadhi ya maeneo aidha kuongeza wachezaji au programu ili kuimarika zaidi kwa sababu kabla ya kukutana kutakuwa na usajili.

“Yanga wanatakiwa kuongeza wachezaji hasa eneo la kiungo na straika mmoja ambaye ataweza kusaidiana na Heritier Makambo, lakini Simba wachezaji wanao wa kutosha wanachotakiwa ni kuboresha programu,” alisema Kashasha.

Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Said Maulid ‘SMG’, alisema straika ya Simba inatakiwa kujilaumu kwa kukosa mabao juzi kwa sababu nafasi walizipata nyingi.

“Yanga wapo kwenye njia sahihi na wanahitaji muda kwa kuwa wanaendelea kuimarika kila siku, ukiangalia katika mchezo ule kwa kushambuliwa kote  hawakuweza kufungwa, walichokifanya ni kitu chanya kwa kuwa Simba wana timu bora,” alisema SMG.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -