Tuesday, October 27, 2020

Okwi kumalizana na Simba Nov 18

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

SIMBA imepania kurudisha heshima yake na katika kufanikisha hilo, uongozi wa klabu hiyo unatarajiwa kumrudisha straika Mganda, Emanuel Okwi, anayetarajiwa kutua jijini Dar es Salaam Novemba 18 na 20, mwaka huu, kusaini rasmi mkataba wa kuichezea miamba hiyo ya Msimbazi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo BINGWA imezipata kutoka ndani ya klabu ya hiyo, zinadai kuwa vigogo wa Simba wamefanikiwa kumaliza dili na klabu yake ya SonderjyskE na sasa staa huyo anaweza kurejea nchini kuongoza kampeni za kurudisha heshima Msimbazi.

Simba wamepanga kutumia dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Novemba 15, mwaka huu, kwa kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kwa kumrudisha straika huyo kipenzi cha wana Msimbazi.

Habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba, ambao ni vinara wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, zinasema kwamba, Okwi, anayekipiga katika klabu ya SonderjykE  ya Denmark, yuko tayari kurejea nchini na ameshafanya mazungumzo na ujumbe maalumu wa Simba uliokwenda nchini Denmark mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, klabu ya SonderjykE imekubali kulipwa kiasi cha Dola 100,000 za Kimarekani, ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 200 za Tanzania.

Katika timu ya SonderjykE, Okwi amekuwa hapati namba, ndiyo maana naye ameona bora arejee kwenye timu yake na viongozi wa Simba wanafanya kila linalowezekana ili kukamilisha zoezi hilo na sasa staa huyo atatua nchini baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.

“Unadhania utani, amini nakwambia, Okwi anatua nchini Novemba 18 ili kusaini mkataba rasmi, lakini asipotua siku hiyo basi Novemba 20 utamuona nchini, huu ndio ukweli na tumepania kuhakikisha mzunguko wa pili tunawasha moto zaidi na kukomaa kileleni hadi mwisho,” kilisema chanzo cha habari hizi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -