Monday, January 18, 2021

OKWI: MAMBO MAZURI YANAKUJA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

WAKATI mashabiki wa soka wakikiona kikosi cha Simba kama tayari kimeiva, mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, amesema wachezaji wakielewana mambo yatakuwa mazuri zaidi.

Okwi ambaye amerejea Simba msimu huu, alitupia bao lake la kwanza juzi  kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar bao 1-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Okwi alisema hivi sasa bado kuna makosa wanayafanya wanapokuwa uwanjani, kwa kuwa wachezaji wengi ni wageni na hawajazoeana lakini muda unavyokwenda hadi kufikia mechi za mashindano watakuwa wameelewana.

“Tunaendelea kuwa makini na maelekezo tunayopewa na kocha wetu ili kupunguza makosa hayo na kuweza kucheza kama timu tofauti na inavyoonekana hivi sasa,” alisema Okwi.

Kuhusu mechi waliyocheza na Mtibwa alisema amefurahishwa na kitendo cha kufunga bao la ushindi na inatokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa wachezaji wenzake.

“Ushirikiano uliopo kwa wachezaji utaifanya Simba kuwa bora zaidi ya hapa na mazoezi tutakayoendelea kufanya  tukiwa kambini Zanzibar, yatatufanya tuelewane na kucheza kama timu,” alisema.

Mechi ya Mtibwa Sugar inaifanya Simba kufikisha jumla ya michezo mitano ya kirafiki ambapo miwili walicheza wakiwa kambini Afrika Kusini.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -