Tuesday, October 27, 2020

OKWI NJIA NYEUPEE SIMBA

Must Read

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika...

NA HUSSEIN OMAR

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, sasa njia yake ya kurejea Simba ni nyeupe, baada ya kuvunja mkataba na klabu yake ya  Sonderjyske Fodbold inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.

Okwi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na ndiyo iliyomuuza katika klabu hiyo ya Denmark, anaweza kusajiliwa na Wekundu hao wa Msimbazi wakati wowote kama mchezaji huru kwa kuwa Simba inayo nafasi moja ya mchezaji wa kimataifa baada ya kuvunja mkataba na kumtoa mshambuliaji wake, Frendrick Bragnon, kwenda nchini Oman.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Simba  katika msimu wa 2009 akitokea SC Villa ya Uganda  na msimu wa 2012, alipigwa bei katika klabu ya Etoile de Sahel ya Tunisia, ambako alishindwa kuitumikia timu hiyo kutokana na mgogoro ulioibuka baina yake na mwajiri wake.

Hata hiyo, Okwi alirejea kuchezea SC Villa kwa muda wa miezi sita akisuburi suala lake kushughulikiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya Etoile kukiuka sehemu ya kipengele cha mkataba wake.

Baadaye, Okwi alisajiliwa na Yanga katika msimu wa 2013/14 wa dirisha dogo la Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini alishindwa kuendelea kuitumikia kutokana na kukiukwa kwa vipengele vya mkataba.

Okwi alirejea Simba msimu uliofuata na Julai mwaka 2015, alijiunga na Sonderjyske, baada ya kusaini mkataba wa mda mrefu hadi mwaka 2020 ambao hakucheza kwa kiwango cha juu, kitu ambacho kimefikia pande hizo mbili kukubaliana kuvunja mkataba.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Michezo klabuni hapo, Jorgen Haysen, hatua hiyo imekuja baada ya Okwi kushindwa kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

“Okwi hajajihakikishia namba kwenye kikosi chetu cha kwanza na hajaonekana kuimarika. Baada ya makubaliano ya pande mbili, tumekubaliana kuachana. Namtakia kila la kheri,” alisema bosi huyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema wanatarajia kumsajili Okwi katika kikosi cha Simba.

Kaburu alisema baada ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara, Desemba 15, mwaka huu kwa sasa hawawezi kumsajili kwa kuwa kanuni haziruhusu.

“Tumeona taarifa ya Okwi kuvunja mkataba na klabu yake, lakini kanuni za usajili haziruhusu hata kama tukimpata leo, uhamisho wa kimataifa utagoma na kile kipengele cha mchezaji kulinda kipaji, kanuni zinasema mkataba unapoisha si kuvunjwa hivyo mpaka dirisha kubwa la Juni,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Manispaa...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu mbele ya Yanga, licha ya...

Kaze amuibua Zahera, aionya Simba

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema aina ya mpira unaocheza kwa sasa...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -