Monday, November 30, 2020

OKWI KUREJEA SIMBA RASMI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA


HATIMAYE juhudi za Simba kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi, zimefanikiwa na anawezekana kuwamo katika kikosi kitakachocheza na mahasimu wao Yanga, Febuari 18, mwaka huu au hata kama mchezo huo utasogezwa mbele.

Okwi anarejea Tanzania kama mchezaji huru, baada ya kuachana na klabu yake ya Sonderjyske ya nchini Denmark ambako mwanzoni aliuzwa na Simba.

Akizungumza na BINGWA, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema tayari wameanza mazungumzo ya awali na straika huyo ili aweze kutua kama mchezaji huru hapa nchini.

“Tumeanza mazungumzo tayari, atakuja kama mchezaji huru, hivyo tunaendelea kuangalia kama inawezekana katika mchezo dhidi ya Yanga, Febuari 18 awe dimbani,” alisema.

Pia aliongeza kwamba mazungumzo yao na Okwi yatategemea kauli ya kocha wao, Joseph Omog, ambaye atakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya kumsajili mchezaji huyo.

“Lazima Omog aamue kwa kuwa yeye ndiye kocha wetu, hivyo hatuwezi kufanya lolote bila ya kauli yake,” alisema.

BINGWA lilimtafuta kocha huyo wa Simba, Omog ili kujua mipango yake na kama atamhitaji mshambuliaji huyo ambapo alisema atafutwe baadaye lakini hakuweza kupatikana tena.

“Nitafute baada ya saa mbili, kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote kinachohusu mshambuliaji huyo,” alisema.

Kwa mara ya kwanza Okwi alitua Simba mwaka 2009 akitokea Sports Villa ya Uganda, kabla ya kuuzwa Etoile de Sahel ya Tunisi mwaka 2012.

Aliondoka kwenye klabu hiyo ya Etoile de Sahel, baada ya kuibuka mgogoro kati yake na mwajiri wake na kurejea Villa kwa muda wa miezi sita. Ambapo alikuwa akisubiria suala lake kushughulikiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya Etoile kukiuka sehemu ya kipengele cha mkataba wake.

Msimu wa 2013/14, Okwi alisajiliwa na Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini alishindwa kuendelea kuitumikia klabu baada ya kukiukwa kwa vipengele vya mkataba na baadaye kurejea Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -