Wednesday, January 20, 2021

OKWI ‘UNSTOPPABLE’

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

EMMANUEL Okwi jana aliendelea kuthibitisha kuwa yeye si muhenga (mkongwe) katika suala zima la usakataji kabumbu, baada ya kuiwezesha timu yake ya Simba kushinda mabao 3-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Okwi, aliyerejea Simba msimu huu tangu alipoondoka misimu miwili iliyopita, alifunga mabao mawili, huku jingine likiwekwa kimiani na John Bocco, kuiwezesha timu yao kufikisha pointi saba ndani ya mechi tatu.

Mabao hayo ya Okwi yamemwezesha kufikisha mabao sita ndani ya mechi zake mbili za Ligi Kuu Bara, ikiwa ni baada ya ‘kutupia’ manne walipovaana na Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza wa ligi Agosti 26, mwaka huu.

Kwa upande wao, kipigo cha jana kimeiacha Mwadui na pointi zake tatu, baada ya kushinda mechi moja na kupoteza mbili.

Akiitumikia Simba katika mchezo wake wa pili wa ligi baada ya kukosa ule wa raundi ya pili dhidi ya Azam wiki iliyopita, Okwi hakufanya ajizi, alitumia dakika 18 tu tangu aingie uwanjani kuipa timu yake bao la kwanza, kutokana na shuti la guu la kulia lililotinga moja kwa moja nyavuni na kumwacha kipa Jacob Massawe akiwa hana la kufanya.

Bao hilo lilitokana na kazi nzuri iliyofanywa na winga wa Simba, Shiza Kichuya.

Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 67, baada ya kupiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja nyavuni, akipokea pasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Dakika tano baadaye, John Bocco, ambaye naye ametua Msimbazi msimu huu akitokea Azam, aliipatia Simba bao la pili, baada ya kuupiga mpira kwa ufundi akiwa nje kidogo ya 18, ikiwa ni baada ya kumhadaa beki mmoja wa Mwadui.

Kwa ujumla, mchezo huo wa jana ulikuwa ni mkali ambapo timu zote zilionyesha shauku ya kutoka uwanjani na ushindi kutokana na kukianza kipute hicho kwa kasi ya aina yake.

Mwadui ndio walioanza kufika langoni mwa Simba, ambapo dakika ya nne, Hassan Kabunda alipiga shuti kali lililotoka nje, ikiwa ni baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Gerard Mathias.

Dakika tatu baadaye, Simba walijibu shambulizi hilo, lakini mabeki wa Mwadui walikaa imara kuondosha hatari hiyo.

Mwadui walifanya shambulizi jingine kali dakika ya 12, baada ya Abdallah Seseme kupiga mpira mrefu ambapo wakati wengi wakiamini unakwenda moja kwa moja nyavuni, kipa wa Simba, Aishi Manula, aliokoa.

Simba nusura wapate bao dakika ya 16, baada ya Okwi kupiga mpira wa adhabu kutokana na mshambuliaji huyo kufanyiwa madhambi, lakini shuti lake lilipaa.

Dakika ya 18 Mwadui walikosa bao, baada ya Awadhi Juma kupokea pasi ya Evarist Mjwahuki na kupiga shuti kali ambalo hata hivyo, lilitoka sentimita chache kutoka kwenye lango la Simba.

Mghana wa Simba, Nicholas Gyan, alikaribia kuifungia timu yake bao dakika ya 24, lakini alishindwa kuitumia nafasi ya wazi aliyopata, baada ya kupiga shuti lililoishia mikononi mwa kipa Massawe.

Dakika ya 25, Kichuya aliachia shuti kali lililogonga mwamba na mpira kurejea uwanjani, ikiwa ni baada ya kuwazunguka mabeki wa Mwadui kutokana na krosi ya Okwi.

Kuona mambo yanaelekea kuwa mabaya kwao, Mwadui walifanya mabadiliko dakika ya 34, kwa kumtoa Gerard Mathias na nafasi yake kuchukuliwa na Benedicto Mwampyate.

Bocco nusura aipatie Simba bao dakika ya 40, ambapo akiwa ndani ya 18, alichelewa kumalizia pasi safi kutoka kwa Okwi, ‘muvu’ hiyo ikiwa imeanzia kwa Gyan.

Dakika ya 63, Kabunda alipiga shuti lililopaa, ikiwa ni baada ya kupokea krosi ya Sesseme.

Mwamuzi wa mchezo huo, Emmanuel Mwandembwa, alimwonyesha kadi ya njano Abdallah Mfuko dakika ya 65, kwa kumfanyia madhambi Bocco.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu hadi mwamuzi Mwandembwa alipopuliza kipyenga cha mwisho, huku Simba wakiibuka kidedea kwa ushindi huo wa mabao 3-0.

Simba: Aishi Manula, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Jjuuko Murushid, Salim Mbonde, James Kotei, Emmanuel Okwi, Mzamiru Yassin/Jonas Mkude dk77, John Bocco, Nicholas Gyan/Mwinyi Kazimoto dk60 na Shiza Kichuya.

Mwadui FC: Anold Massawe, Malika Ndeule, David Luhende, Revocatus Mgunga, Abdallah Mfuko, Razack Khalfan/Moris Malaki dk79, Abdallah Sesseme, Awadhi Juma/Awesu Ali dk69, Evarist Mjwahuki, Gerard Mathias/Benedicto Mwampyate na Hassan Kabunda.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -