Tuesday, October 20, 2020

OMMY DIMPOZ HAWEZI KUSAHAU ALIVYOSWEKWA JELA MAREKANI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA BEATRICE KAIZA


KAMA tulivyoahidi kumleta kwenu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo, ambaye jina lake la kutafutia ugali anafahamika kama Ommy Dimpoz, staa huyu amekutana na Jiachie na Staa Wako na kujibu maswali yenu na kupokea ushauri mliompatia.

Swali: Bibi Kidude wa Mwakidira Tanga, naomba kujua ukweli kutoka kwa  Ommy Dimpoz, kipindi kile unatayarisha wimbo wa ‘Wanjera’ kulikuwa na tetesi za kutoka kimapenzi na Wema Sepetu, je, ni kweli ulikuwa na uhusiano naye wa  kimapenzi?

Jibu: Hapana, zilikuwa ni tetesi tu, pia watu walisahau kama Wema ni mwigizaji na ana uhuru wa kufanya chochote.

Katika utayarishaji wa kazi kama ile ni lazima kuwe na kitu ambacho kitafanya watu kusubiri kwa hamu kazi yako, zile picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa ni maandalizi ya video ya Wanjera.

Zaidi ya hapo, Wema ni mshkaji wangu wa karibu, nampenda kwa sababu amekuwa akinisapoti kazi zangu.

Swali: Mama Atu wa Kawe, Dar es Salaam, ni kitu gani kilisababisha ukaingia kwenye bifu na Diamond?

Jibu: Sina bifu na msanii yeyote yule katika sekta hii ya sanaa.

Swali: Letisia Samweli wa Dar es Salaam, kitu gani kilikufanya hadi ukamsainisha msanii chipukizi, Nedy Music katika lebo yako ya PKP?

Jibu: Nedy Music ni msanii chipukizi ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Usiende Mbali’.

Uwezo wake ndio ulionishawishi hadi  nikaamua kumsainisha kwenye lebo yangu ya PKP, pia ana nidhamu na mwonekano mzuri, kifupi amekaa kibiashara.

Swali: Mwamadi Speni wa Dar es Salaam, baada ya Nedy Music ni nani  umepanga kumsainisha PKP?

Jibu: Kuna wasanii wengi ambao wanatamani kusainiwa kwenye lebo ya PKP, lakini ninachoweza kukudokeza ni kwamba hivi karibuni tutamtambulisha msanii mpya wa kike.

Swali: Naitwa Mudy wa Tabora, Ommy Dimpoz, baada ya Kajiandae mashabiki wako tutegemee nini kutoka kwako?

Jibu: Mashabiki zangu wategemee vitu vizuri kutoka kwangu, pia kutakuwa na kolabo ambazo nimefanya na wasanii wa nje ya nchi.

Swali: Naitwa Erick Samwel wa Dar es Salaam, Ommy Dimpoz, vipi mbona hadi leo ujatoa nguo za PKP?

Jibu: Nilikuwa na mpango huo, lakini bado nafikiria njia sahihi ya kuweza kuhakikisha hakuna wajanja watakaoweza kuharibu biashara yangu kwa kutoa bidhaa feki.

Swali: Mariam Musa wa Dar es Salaam, unawaambia nini watu ambao wanatumia muda wao kukutukana kwenye mitandao ya kijamii?

Jibu: Hakuna haja ya kuwajengea chuki watu wanaojifanya hawakupendi kwa sababu zao binafsi.

Mimi nawaombea tu kwa Mungu wazidi kufanikiwa kwenye maisha yao.

Swali: Naitwa Omary Juma wa Dar es Salaam, ni kweli ulilala jela nchini Marekani na kama ni kweli ulikamatwa kwa kosa gani?

Jibu: Ndio nimewahi kulala jela nchini Marekani ambako nilikamatwa kwa kosa la kumiliki viza yenye mapungufu.

Swali: Kitu gani kilikushawishi hadi ukaamua kufanya kazi na Ali Kiba na si msanii mwingine kwenye wimbo wako mpya wa Kajiandae?

Jibu: Si mara yangu ya kwanza kufanya kazi na Ali Kiba, niliwahi kumshirikisha Ali Kiba kwenye wimbo wangu Nai Nai ambao ulinitambulisha katika tasnia ya muziki na kufanya jina langu kukuwa ndani na nje ya nchi.

Kufanya vizuri kwa Nai Nai ilitosha kunishawishi kufanya kazi nyingine na Ali Kiba ili kuwakumbusha mashabiki wetu kuwa tunaweza kufanya tena kazi nzuri zaidi.

Swali: Naitwa Zena Saidi wa Magomeni, Dar es Salaam. Ommy Dimpoz ni tukio gani ambalo huwezi kulisahau katika maisha yako?

Jibu: Aaaaah! ‘kicheko’ kituko ambacho siwezi kukisahau katika maisha yangu ni siku ambayo niliswekwa lupango kwa kosa la kutumia vibaya viza ya kusafiria.

Nakumbuka nilikuwa natoka Uingereza kwenda Marekani, viza niliyokuwa nayo ilikuwa inaonyesha nakwenda kutalii na si kwenda kufanya kazi kama mwenyeji wangu alivyonidanganya.

 

Swali: Naitwa Konlardy Steven wa Mbeya, Ommy Dimpoz kwanini unapenda kufanya video zako Afrika Kusini?

Jibu: Kwa kweli napendelea kwenda kufanya kazi Afrika Kusini kwakuwa hapa nyumbani mazingira ni  magumu kwenye uandaaji wa video.

Kwa mfano ukitaka kutengeneza video kwenye hoteli kwa hapa Tanzania  unaweza kuchajiwa fedha  nyingi kuliko Afrika Kusini.

Swali: Naitwa Mick Masilva wa Mbagala, Dar es Salaam, nataka kajua Ommy Dimpoz kama una mpenzi na kama yupo mbona sisi mashabiki wako hatumjui, ni sababu gani inayokufanya umfiche?

Jibu: Mpenzi ninaye na tunapendana sana, kuhusu mashabiki zangu kujua mpenzi wangu si kitu cha lazima kwani sipendi wajue maisha yangu binafsi zaidi ya kazi zangu za muziki.

Pongezi: Naitwa Rajabu Adamu wa Singida, hongera kaka Ommy Dimpoz kwa kazi nzuri ya kutoa elimu na burudani kwa jamii.

Jibu: Asante sana Rajabu tuko pamoja.

Swali: Naitwa Augustino Mgonde wa Mbeya, Ommy Dimpoz, ni shabiki wa timu gani kwa hapa Tanzania?

Jibu: Mimi ni shabiki wa timu ya Simba kwa hapa Tanzania.

Ushauri: Naitwa Juma Ndambe wa Jaribu Mpakani, napenda kumshauri Ommy Dimpoz aachane na mambo ya  malumbano na wasanii wenzake kama kutupiana maneno machafu kwenye  mitandao ya kijamii kwani  kutakupotezea mashabiki na kushusha hadhi yako kwa jamii.

Jibu: Asante Juma tupo pamoja sana.

Hawa ni baadhi ya mashabiki wa Ommy Dimpoz waliojitokeza kumuuliza maswali na kumpa pongezi na ushauri.

Katika toleo lijalo tunamleta kwenu mrembo, Lulu Mkongwa ‘Amber Lulu’  ambaye amejipatia umaarufu  kupitia mitandao ya kijamii hasa Instagram.

Tumia fursa hii kumuuliza maswali ili kukata kiu yako, lakini pia waweza kumpa ushauri na pongezi kwa kutuma ujumbe kupitia namba ya simu iliyoko hapa  juu na majibu yatapatikana hapa hapa katika toleo la Jumanne ya wiki ijayo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -