Thursday, December 3, 2020

OMOG ABADILI ‘FOMESHENI’ SIMBA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

JACKLINE LAIZER, ARUSHA NA SAADA SALIM

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amebadili ‘fomesheni’ ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Madini, utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Akizungumza na BINGWA jana, Omog alisema amelazimika kubadili fomesheni, baada ya kuona ubovu wa viwanja vya mikoani.

Omog alisema wametaka wachezaji wake kucheza na kupiga pasi ndefu badala ya pasi fupi ili waweze kufunga mabao katika mchezo huo na mechi nyingine za Ligi Kuu Bara zitakazocheza Kanda ya Ziwa.

Omog alisema wachezaji wake wanatakiwa kuhakikisha hawatapoteza mpira, kwani mchezo wao dhidi ya Madini ni muhimu kushinda ili kutinga nusu fainali.

Alisema kazi kubwa watakayoifanya ni kuhakikisha viungo wanakuwa makini kutopoteza na kupeleka mashambulizi kwa wapinzani wao.

Omog amewataka wachezaji wake hasa katika safu ya ushambuliaji kuwa makini katika ufungaji.

Omog alisema kazi kubwa aliyoifanya ni kuhakikisha mabeki, washambuliaji na viungo wanafanya kazi nzuri ya kutimiza majukumu yao uwanjani.

Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, amesema hawataudharau mchezo huo.

Mayanja alisema wana kiu ya kuendeleza ushindi katika michuano yoyote ya kombe hilo  ili aweze kuchukua ubingwa wa msimu huu.

Alisema kwa sasa kikosi chake kipo katika hali nzuri isipokuwa beki wa timu hiyo, Method Mwanjale.

Mayanja alisema kukosekana kwa beki huyo hakutawazuia kuibuka na ushindi, kwani wamejipanga vilivyo kuwashikisha adabu wapinzani wao.

“Unajua hakuna timu ndogo kwenye mashindano na hatuwezi kuidharau timu yoyote, kwani mpaka imefikia hatua hii ujue ni nzuri na mchezo utakuwa wa ushindani, hivyo tumejipanga vyema kuwaondoa katika michuano hii,” alisema Mayanja.

Alisema wana kila sababu ya kufika mbali msimu huu katika mashindano yoyote yale yaliyo mbele yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -