Saturday, November 28, 2020

OMOG ABADILI GIA KUSAKA UBINGWA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM

BAADA ya kupoteza pointi muhimu katika mchezo na Kagera Sugar, kocha mkuu wa Simba Mcameroon, Joseph Omog, ameamua kubadili gia ili kuhakikisha anaupata ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Simba ambayo itacheza na Mbao FC Jumatatu ijayo, inahitaji ushindi katika mechi hiyo na mechi nyingine zinazofuata ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa walioukosa kwa miaka minne sasa.

Katika maandalizi ya mchezo wao huo, Omog ameonekana kubadilisha mbinu kwani kwenye mazoezi ya timu hiyo ameonesha hataki masihara kwa kuwanoa washambuliaji wake hasa katika suala ya umakini wa kulenga lango jambo ambalo amedai limekuwa likiwagharimu sana.

“Tumepoteza nafasi nyingi kwenye mchezo na Kagera, kila aliyepata nafasi hakuitumia vyema, kwa hiyo wachezaji wote wanaangukia kwenye zoezi moja kwanza la kufunga mabao, kisha mambo mengine yatakuja kutokana na mujukumu yao uwanjani,” alisema Omog.

Kwa upande wake, Meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alisema kikosi chao kinaendelea vizuri na wanajipanga kuhakikisha wanapata pointi muhimu katika mchezo wao dhidi ya Mbao.

Alisema Omog anafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wao na Kagera ili yasijitokeze katika mchezo unaofuata hasa kwa kuwapika wachezaji wake namna ya kufunga mabao.

“Simba ilitengeneza nafasi nyingi sana, lakini kila aliyepata nafasi hakuitumia vizuri, kwa hiyo hilo kocha analifanyia kazi kwa nguvu zote kuelekea katika mechi zetu zilizobakia,” alisema Mgosi.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa timu hiyo, Laudit Mavugo, alisema kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata sasa wanapewa mazoezi ya nguvu na kocha kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kuhakikisha wanapata ushindi.

Alisema kwa sasa wanahakikisha wanafanya vizuri katika michezo iliyobakia hasa kupata pointi zote 15 wakianzia mchezo wao dhidi ya Mbao ambapo watapambana kupata ushindi.

“Kwa sasa kocha anatuandaa vyema, wachezaji tunahakikisha hatutawaangusha Wanasimba kwani tutafanya vizuri katika mchezo wetu ujao na mingine,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -