Friday, December 4, 2020

OMOG AIKESHEA YANGA ZENJI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA SALMA MPELI

SIMBA inashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kwenye Uwanja wa Amaan, kisiwani Unguja, lakini akili ya Kocha Mkuu wake, Joseph Omog,  inaliwaza pambano la mahasimu wake wa jadi, Yanga, Februari 17.

Omog amesema kwa sasa Kombe la Mapinduzi linampa muda wa kuangalia kikosi chake na kuona namna atakavyowaacha mbali wapinzani wao wa jadi Yanga kwenye msimamo, lakini pia kuona jinsi ya kupata ushindi dhidi yao kwenye mechi ya marudiano.

Kocha huyo raia wa Cameroon ameliambia BINGWA kuwa hajaenda visiwani humo kulala usingizi, kwani anaitumia michuano hiyo kufua makali ya wachezaji wake ili kuongoza kasi ya kushinda mechi za Ligi Kuu Bara na baadaye wachukue ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.

Omog alisema uwiano wa tofauti ya  pointi nne na Yanga ni mdogo, hivyo anataka kuendelea kuwaacha mbali ili awe na uhakika wa kutwaa ubingwa huo.

Alisema pamoja na kutambua umuhimu wa kuchukua Kombe la Mapinduzi, lakini yuko makini kuhakikisha wachezaji wake wanaongeza kiwango kupitia michuano hiyo.

“Tukiwafunga Yanga tutaendelea kuwaacha zaidi, akili yangu ni kushinda mechi nyingine niendelee kuwaacha lakini pia kuona namna ambavyo nitawafunga Yanga,” alisema.

Omog alisema malengo yao ni kuona wanashinda mataji yote hivyo atahakikisha anakuwa makini hasa katika kuwanoa wachezaji wake ili kila mmoja aweze kuonyesha soka safi.

Alisema anafurahishwa na kiwango kinachoonyeshwa na wachezaji wake akiwamo beki wake, Abdi Banda, ambaye kwa sasa amekuwa akimwazisha katika kikosi chake cha kwanza.

Alisema anaendelea kuwafua wachezaji waliojiunga na kikosi hicho katika dirisha dogo la usajili la ligi hiyo akiwamo Pastory Athanas kutoka Stand United na Waghana, James Kotei na Daniel Agyei.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -