Friday, December 4, 2020

Omog akabidhiwa jukumu lingine Simba

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

SALMA MPELI NA ZAITUNI KIBWANA,

SIKU moja baada ya Simba kumleta nchini kipa wa Medeama, Daniel Agyei, Wekundu hao wa Msimbazi wamesema kuwa rungu la kukata wachezaji, akiwamo kipa mmoja ameachiwa kocha wao, Joseph Omog.

Agyei ameletwa ili kuongeza nguvu na kumsaidia Vincent Angban ambaye alionekana kukosa mpinzani katika kikosi hicho.

Akizungumza na BINGWA, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili, Kassim Dewji, alisema jukumu la kukata kipa mmoja  na wachezaji wengine wasiohitajika wamemwachia Omog.

“Utaratibu wetu upo tofauti kidogo, Omog alitaka kipa na sisi tumemleta nchini, hivyo suala la nani anaachwa hilo naomba tumsubiri arudi kocha mwenyewe atatuambia,” alisema.

Alisema kipa huyo atafanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kuingia naye mkataba mpya wa kuanza kazi rasmi ya kucheza kwenye kikosi hicho.

“Kesho (leo) tutamfanyia vipimo Agyei na baada ya hapo tutamsajili na kumsubiri Omog ambaye bado yupo mapumzikoni nchini Cameroon,” alisema.

Licha ya Kassim kutotaja nyota atakayekatwa kwenye kikosi hicho, BINGWA inatambua nyota Mussa Ndusha ambaye hajapata nafasi mzunguko wa kwanza na beki Besala Bukungu, hawapo salama kwenye kikosi hicho kwa sasa.

Ujio wa Agyei unazidisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwenye kikosi hicho ambacho tayari idadi hiyo walishaitimiza.

Katika hatua nyingine, Rais wa Simba, Evans Aveva, anatarajiwa kukutana na viongozi wa matawi wa klabu hiyo kesho  kwa lengo la kuzungumzia maandalizi ya mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 11, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa  Polisi Oysterbay.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -