Sunday, January 17, 2021

OMOG AMTAFUTA UBAYA CANNAVARO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA EZEKIEL TENDWA

KAMA mabeki wa Yanga wakiongozwa na nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, hawatajipanga sawasawa, wanaweza wakapata aibu ya mwaka kutokana na hicho kinachofanywa na Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog.

Timu hizo hasimu zinatarajiwa kukutana Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo zote zimekwenda kujificha nje ya jiji hilo, Simba wakiwa Unguja na Yanga Pemba, kuhakikisha wananoa silaha zao.

Safu hiyo ya ulinzi ya Yanga chini ya Cannavaro na wenzake, Kelvin Yondani, Andrew Vincent na Abdallah Shaibu ‘Ninja’, anatakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanagundua mbinu hizo za Omog, vinginevyo aibu itawapata.

Anachokifanya Omog ni kutengeneza kombinesheni ya ajabu akianzia pale katikati ya uwanja, ambapo Haruna Niyonzima na Said Ndemla, wamepewa jukumu la kuhakikisha wanafanya udambwiudambwi wao kama kawaida kuwarahisishia kazi Emmanuel Okwi na John Bocco watakaosimama mbele.

Okwi na Bocco wamesukwa upya kuhakikisha wanafunga mabao mengi na jukumu la kuwalisha mipira, wameachiwa viungo wanaoongozwa na Niyonzima ambaye anaonekana kuelewana vizuri sana na Ndemla.

Mbali ya Ndemla, pia Niyonzima amekuwa akielewana na Jonas Mkude ambaye katika mechi za kirafiki amekuwa akitokea benchi, huku pia Mzamiru Yassin naye akitumiwa kama silaha yenye sumu kali, hiyo ikimaanisha kwamba Cannavaro na wenzake wanatakiwa kuomba Mungu mchana na usiku wachezaji hao waamke vibaya siku hiyo.

Jambo la kutisha zaidi kwa mabeki hao wa Yanga ni kwamba, Omog pia amemsuka vikali winga wake Shiza Kichuya, ambaye siku zote anapokutana na Wanajangwani hao anakuwa kama anawashwa na miguu akitaka tu kufunga, huku mpambanaji Mohamed Ibrahim ‘Mo’, naye akiwa ameshalishwa upupu na kilichobakia ni kuupuliza tu.

Kutokana na jinsi alivyoyaangalia mazoezi ya timu yake na namna akina Niyonzima wanavyopokea maelekezo ya kocha wao, mkuu wa kambi ya Simba iliyopo Unguja, Abdul Mshangama, amewaambia mashabiki wao wajiandae kwa furaha kwani ushindi siku hiyo ni lazima.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -