Monday, November 23, 2020

OMOG ANA UHAKIKA WA KUICHAPA MBEYA CITY

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM,

KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amesema licha ya kutowaona Mbeya City wakicheza katika siku za hivi karibuni, lakini ana imani watafungika katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Simba ipo kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 54, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 52 na nafasi ya tatu inashikiliwa na Azam FC wakiwa wamejikusanyia pointi 41.

Omong ameliambia BINGWA kwamba hivi karibuni hajawaona wapinzani wao, lakini ubora wa kikosi chake kwa sasa unampa uhakika wa kushinda katika mchezo huo ambo ni muhimu sana kwao.

Alisema ushindani uliopo kwenye mbio za ubingwa unamfanya kuwa makini kuhakikisha anajipanga kushinda kila mechi ili kuendelea kubaki katika nafasi waliyopo sasa.

Kocha huyo alisema hajapata nafasi ya kuwaona wapinzani wao kwa hivi karibuni, lakini kulingana na maandalizi ya kikosi chake, wamejipanga kushinda mchezo huo na mingine iliyobakia.

“Tumebakisha mechi saba na hakuna timu rahisi katika hizo, mbaya zaidi hizi timu za chini huwa zinakamia, tumejipanga kufanya vizuri katika mchezo wetu huo,” alisema.

Omog alisema lengo lake kubwa ni kuhakikisha wanapata pointi nyingine tatu kutoka kwa wapinzani wao ili kujihakikishia kubaki katika nafasi hiyo.

“Hatujabweteka na ushindi tuliopata Jumamosi iliyopita, nadhani mchezo huu ujao ni mgumu kuliko Yanga, wachezaji wangu wako fiti na tayari kwa ajili ya mapambano,” alisema Omog.

Akizungumzia mrithi atakayecheza nafasi ya beki wao, Javier Bukungu aliyepewa kadi nyekundu, kocha huyo alisema ana imani na wachezaji waliopo kwani wana uwezo wa kucheza vizuri sana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -