Tuesday, November 24, 2020

OMOG ASHIKWA UCHAWI SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

SAADA SALIM NA ZAINAB IDDY ,

SIKU chache baada ya Simba kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kulala bao 1-0 na Azam FC, zigo la lawama limemwangukia kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Omog.

Pamoja na mambo mengine mengi, kudorora kwa Simba kumedaiwa kusababishwa na kitendo cha Omog kushindwa kupata kikosi cha kwanza (First Eleven), lakini pia mifumo anayoitumia ambayo haiiwezeshi timu hiyo kupata mabao mengi.

Omog ambaye anasifika kutokana na mfumo wake wa kujaza viungo wengi na kucheza soka la kujilinda, mbinu zake zimeonekana kushindwa kufurukuta kwa wakati huu ambao soka linazidi kubadilika kulingana na wakati.

Itakumbukwa kuwa Omog wakati anaingia Azam FC msimu wa 2013/14, aliutumia mfumo huo na timu hiyo kufanikiwa kubeba ubingwa bila ya kufungwa.

Pia, Omog amekuwa akilaumiwa katika suala zima la upangaji kikosi kwa kuwaweka benchi baadhi ya wachezaji muhimu kama Laudit Mavugo, Shiza Kichuya, Said Ndemla na wengineo na badala yake kuwaingiza kipindi cha pili.

Ukiachana na Omog, pia kukosekana kwa Mohammed Ibrahim ‘Mo’, kumetajwa kuchangia kuishusha Simba kileleni kwani wakati akiwa dimbani, alikuwa akitoa mchango mkubwa wa kuiunganisha timu, zaidi ikiwa ni safu ya ushambuliaji.

Mo alijenga kombinesheni nzuri na Mzamiru Yassini ambapo alikuwa akifanya vizuri na hatimaye kuifungia mabao Simba, hivyo kutokuwepo kwake kikosini kutokana na majeraha, kumetajwa kuiathiri timu hiyo.

Kutokana na yote hayo, mashabiki wa Simba wametoa yao ya moyoni wakilitupia lawama benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla kwa kushindwa kutimiza majukumu yao.

“Simba haikuwa makini wakati wa dirisha dogo kwa kufanya usajili sahihi wa washambulizi kwani wale waliokuwapo sasa hakuna mwenye msaada na timu. Kibaya zaidi, wamemtoa Fredick Blagnon ambaye alionekana kuwa na uwezo, hili ni tatizo lazima litafutiwe tiba,” alisema mmoja wa wanachama hao, Masoud Ally wa tawi la Tabata Relini, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -