Saturday, October 31, 2020

Omog ataja siri yake na Jjuuko Murshid

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM,

KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amevunja ukimya na kutaja kile kilichokuwa kinamfanya asimtumie mara kwa mara beki wake wa kati, Jjuuko Murshid.

Tangu kuanza kwa msimu huu Murshid amekuwa hapewi nafasi ya kutosha katika kikosi cha Simba, kwani kocha wa timu hiyo, Omog amekuwa akimpendelea zaidi beki Novaty Lufunga.

Hatua ya Omog imekuwa ikipingwa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wanaoamini Jjuuko ambaye pia ni beki wa kutumainiwa wa Uganda ni bora zaidi ya Lufunga.

Lufunga ametengeneza kombinesheni kali katika beki safi ya ulinzi ya Simba pamoja na mabeki wengine wa timu hiyo, Method Mwanjali, Mohameed Hussein na Javier Bokungu.

Omog ameliambia BINGWA kuwa anafahamu Jjuuko ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda ‘Cranes’, hivyo kutomtumia kwake mara kwa mara na badala yake kumpa nafasi zaidi Lufunga kulilenga kuepuka kuiathiri timu pale atakapokwenda kushiriki Afcon.

Alisema anaimani Lufunga ataendelea kufanya vizuri hata pale Jjuuko atakapokosekana katika kikosi chake.

“Nina wachezaji wazuri na katika kila nafasi ina watu watatu, nilitambua mapema kwamba tutakuja kumkosa Jjuuko katika baadhi ya mechi na ndiyo maana nikatengeneza kombinesheni ya mabeki wengi,” alisema.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari limeshatoa ratiba ya makundi ya michuano hiyo ya AFCON, huku Uganda ikipangwa kundi D pamoja na nchi za Ghana, Mali na Misri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -