Friday, October 23, 2020

OMOG AWAFUNGIA KAZI MAVUGO, AJIB

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SALMA MPELI

KOCHA wa Simba, Joseph Omog,  ameamua kuwafungia kazi washambuliaji wake, Laudit Mavugo, Pastory Athanas na Ibrahim Ajib, kwa kuwatengea mazoezi maalumu kwa ajili ya kupachika mabao.

Simba wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Azam itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru.

Kufuatia hali hiyo, Omog ameona ni vema kuanza kuinoa zaidi safu yake ya ushambuliaji ili kuwa tishio kwenye mchezo wao na Azam, ambapo ushindi huo utaendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Omog alisema maandalizi kuelekea mchezo huo yapo vizuri, lakini ameona umuhimu kuanza na safu yake ya ushambuliaji, kutokana na kushindwa kufunga mabao mengi na kuwategemea zaidi viungo wao kwenye ufungaji.

“Maandalizi yanaendelea kama mlivyoona, lakini kesho asubuhi (jana asubuhi), nitaanza na kuwanoa washambuliaji na baadaye jioni tutakuwa na mazoezi ya pamoja,” alisema.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walimvaa meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’, wakihoji tatizo sugu la washambuliaji.

Baadhi ya mashabiki hao walitaka meneja huyo kumfikishia ujumbe kocha wao na kubadili mfumo ili kuangalia mfumo bora utakaowezesha kupata mabao mengi.

Katika mchezo wao huo wa Jumamosi dhidi ya Azam, huenda Simba wakamkosa kiungo wao, Mohamed Ibrahim ‘Mo’, ambaye ana majeruhi ya goti aliyoyapata katika michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo wa nusu fainali dhidi ya Yanga.

Kutokana na majeruhi hayo, tayari Mo ameshazikosa mechi tatu ambazo ni fainali ya Kombe la Mapinduzi waliyofungwa 1-0 na

Azam, mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara  dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi ya Kombe la FA dhidi ya Polisi Dar.

Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, alisema mchezaji huyo anaendelea na matibabu, ingawa ameanza mazoezi madogo madogo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -