Sunday, January 17, 2021

OMOG: NIPO TAYARI KUTIMULIWA SIMBA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HUSSEIN OMAR

SIKU chache baada ya taarifa kwamba uongozi wa Simba umempa mechi nne Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, amefunguka akisema yupo tayari kwa lolote katika klabu hiyo ya Msimbazi.

Omog ametoa kauli hiyo baada ya uongozi na mashabiki wa Simba kumtupia lawama kwamba ameshindwa kuifundisha timu hiyo kutokana na kutoridhika na kiwango kinachoonyeshwa tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya.

Akizungumza na BINGWA jana, Omog alisema kuwa yeye kama mwajiriwa wa Simba, amejiandaa kisaikolojia kwa lolote litakalotokea ndani ya klabu hiyo ambayo msimu huu imedhamiria kufanya kweli kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kusajili majembe ya ukweli.

Licha ya kuwa na wachezaji wengi wazuri na wenye uwezo, lakini Simba bado imekuwa ikipata ushindi mwembamba kwenye mechi zake mbalimbali za kirafiki na Ngao ya Jamii uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na timu yake kuibuka washindi kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare 0-0 wa dakika 90.

“Kama kocha lazima niwe tayari kufukuzwa hilo naheshimu, lakini pia lazima utambue mimi ni mwajiriwa wa Simba, nimejiandaa kwa kila jambo,” alisema Omog.

Mmoja wa kiongozi wa juu wa klabu hiyo alinukuliwa na BINGWA katikati ya wiki hii kuwa, kocha huyo si mbaya ila anaponzwa na mbinu na mfumo anaoutumia pamoja na majeruhi waliopo kwenye timu ambao kwa asilimia kubwa anawategemea.

Simba wanafungua ligi leo kwa kuvaana na Ruvu Shooting kabla ya kuwavaa Azam FC, Mwadui FC na Mbao FC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -