Friday, December 4, 2020

ORIGI NI ‘PLAN B’ ILIYOIBUKA LIVERPOOL WAKATI SAHIHI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MERSEYSIDE, Liverpool

NI asilimia ndogo ya mashabiki wa Liverpool ambao walifurahia kusikia kuwa kiungo wao, Philippe Coutinho, atakosekana kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha aliyoyapata.

Mbrazil huyo ameanza msimu huu kwa kiwango cha hali ya juu, lakini hiyo si sababu pekee itakayoiweka Liverpool kwenye hali ngumu inayotabiriwa kutokea baadaye.

Unajua kwanini? Tulia tukujuze.

Kocha wao, Jurgen Klopp, amefaulu katika suala zima la mfumo na mikakati mipya ndani ya Liverpool, hasa washambuliaji wake ambao wameibeba hadi kutinga ‘Top Four’ ya Ligi Kuu England.

Coutinho pia ni mmoja wa washambuliaji walioibeba timu hiyo na kwa inavyoonekana, anaweza kuukosa mchezo wa mwisho kwa mwaka huu dhidi ya Man City. Ni pigo kwa sababu City wameshindwa kuzuia mateso ya Coutinho, iwe ni Anfield, Etihad au Wembley.

Liverpool sasa itakuwa na jukumu la kuikabili City bila ya silaha yao muhimu, lakini jambo la kutia moyo ni mchezaji aliyeingia kuchukua nafasi yake dhidi ya Sunderland, Divock Origi, alifunga bao moja na kufunga lingine dhidi ya Leeds kwenye mchezo wa EFL mapema wiki hii.

Kwa lengo la kuufanya mfumo huo uendelee kutumika, Origi huenda akatumika kama mshambuliaji wa kati na Klopp pia anaweza kuamua kumtumia Roberto Firmino pembeni kwa ajili ya kutengeneza nafasi nyingi zaidi.

Daniel Sturridge anaweza kutumika, lakini Origi ndiye anayeangaliwa zaidi kama mtu sahihi wa kuanza kikosi cha kwanza wakati Coutinho akiendelea kuuguza jeraha la enka.

Origi ataaminiwa na Klopp kwenye michezo ya ligi kwa mara ya kwanza kwamba atakuwa fiti kufunga mabao na umri wake wa miaka 21 unampa nafasi nzuri ya kutumika hivi sasa, licha ya kupitwa takwimu za mabao na Sturridge.

Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita Klopp aliwashangaza mashabiki wake kwa kumpa nafasi Origi badala ya Sturridge, walipokabiliana na Borussia Dortmund kwenye robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Europa, lakini imani yake ilimlipa kwa kufunga bao moja akiongoza safu ya ushambuliaji.

Mchezo wa marudiano kwa mara nyingine alimpa nafasi na akafunga tena katika ushindi wa kusisimua wa mabao 4-3.

Kama hiyo haitoshi, straika huyo alitupia mabao mengine dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa ligi, mengine matatu dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa Kombe la Capital One, na bao moja dhidi ya Everton, lakini kwa bahati mbaya aliumizwa vibaya na beki Funes Mori kiasi cha kukosa mechi zote zilizosalia.

Halikuwa jambo la kufurahisha, kwani mashabiki wa Liverpool walifurahia mno kiwango chake cha kufunga mabao.

Kwa wakati huu ambao Klopp atakosa huduma za Coutinho, Lallana na Sturridge, ni wazi kuwa kuibuka tena kwa Origi ni habari njema kwake, hasa pia kutokana na kiwango cha Sadio Mane kupungua kidogo tangu alipofunga kwenye ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Watford na akisubiriwa na jukumu la kuiwakilisha timu yake ya taifa ya Senegal kwenye michuano ya Afcon Januari, mwakani, ambapo kutakuwa na mechi mbili za ziada, ikiwemo nusu fainali ya EFL Cup.

Maumivu ya kumkosa Coutinho yanapunguzwa taratibu na jinsi Origi anavyofunga mabao ya muhimu kwenye mechi muhimu. Hata kama nguvu yake haitakuwa kubwa kwenye michezo ijayo, hiyo itakuwa ni furaha kwa Klopp, kwani mikakati yake inaanza kulipa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -